Na: Amina Hezron,Kilombero.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero mkoani
Morogoro Dunstan Kyobya amewaomba Wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo (SUA) kujenga uelewa wa namna sahihi ya kuongeza thamani ya zao la
mpunga pamoja na mbinu za kuongeza tija katika uzalishaji wa zao hilo katika
Wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Dunstan Kyobya akizungumza na wadau wa kilimo pamoja na wataalamu kutoka SUA.
Kyobya ametoa maombi hayo wakati
alipokuwa akifungua Warsha iliyoandaliwa na Watafiti kutoka SUA iliyokutanisha
wadau wa kilimo kwaajili ya kutoa mrejesho wa utafiti uliohusu Utayarishaji
Shirikishi wa Huduma za Hali ya Hewa ili Kuboresha Uhakika wa Chakula, Lishe na
Afya nchini Tanzania.
Amesema bado hajaridhishwa na
kiwango cha uzalishaji wa mpunga katika wilaya yake japokuwa ndiyo wilaya
inayoongoza katika uzalishaji wa zao hilo ambapo Halmashauri ya wilaya ya Mlimba
peke yake ikizalisha vyema inauwezo wa kulisha Tanzania nzima hivyo amewataka
wataalamu kutoka SUA kuelekeza njia sahihi na mbegu bora za kutumika.
“Tunalima tunapata kidogo heka
moja ya shamba la mpunga linaweza kuzalisha gunia 25 lakini nimesoma sehemu
wakati nakuja huku kuwa unaweza kuzalisha mpaka gunia arobaini na tano hadi
hamsini za mpunga kwanini na sisi tusifanye hivyo”, alisema Kyobya.
Akielezea lengo la warsha hiyo na
kuanzishwa kwa Mradi huo Kaimu Mratibu wa Mradi kutoka SUA Dkt. Sylvester Haule amesema ni kuongeza matumizi
ya huduma za hali ya hewa kwa kujifunza jinsi mabadiliko ya hali ya hewa
yanavyoathiri kilimo, mifumo ya chakula na afya pamoja na mienendo ya maamuzi
katika ngazi ya kaya.
Kaimu Mratibu wa Mradi kutoka (SUA) Dkt. Sylvester Haule akiuelezea Mradi kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero.
“Katika Mradi wetu huu tumelenga
kuongeza uwezo wa mamlaka ya hali ya hewa kutoa tabiri zinazokidhi mahitaji ya
wakulima, kuboresha huduma za hali ya hewa na uwasilishaji wake kwa wadau
katika ngazi ya chini kwa kushirikiana na Mamlaka za hali ya hewa,Wizara ya Kilimo,
Wizara ya Afya na Maafisa ugani na Maafisa
afya”, alifafanua Dkt Haule.
Mradi huu wa miaka miwili umekuwa
ukitekelezwa kuanzia mwezi Aprili 2021, na kumalizika 2023 katika Halmashauri
ya Wilaya ya Mlimba na na Mvomero kwa ushirikiano baina ya Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo (SUA), Taasisi ya Michelsen (CMI) ya nchini Norway, Kituo
cha Kimataifa cha Utafiti wa Tabianchi na Mazingira (CICERO) ya Norway, kituo
cha Utafiti cha Norway (NORCE) Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Taasisi
nyinginezo zilizoko Norway.
Mkuu
wa Wilaya ya Kilombero Mhe Dunstan Kyobya na Wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo SUA. |
Viongozi mbalimbali wa Wilaya na Wadau wengine wa kilimo wakisikiliza mawasilisho ya mtokeo ya utafiti. |
Viongozi mbalimbali wa Wilaya na Wadau wengine wa kilimo wakisikiliza mawasilisho ya mtokeo ya utafiti. |
Viongozi mbalimbali wa Wilaya na Wadau wengine wa kilimo wakisikiliza mawasilisho ya mtokeo ya utafiti. |
Viongozi mbalimbali wa Wilaya na Wadau wengine wa kilimo wakisikiliza mawasilisho ya mtokeo ya utafiti. |
0 Comments