Na Josephine Mallango
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
(SUA) kimesaini makubaliano ya ushirikiano na Taasisi 10 kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo
Waziri wa Wizara hiyo Mhe.
Abdallah Hamis Ulega amesema watatumia
vijana madaktari wa mifugo kutoka SUA katika
kampeni ya chanjo kwa mifugo nchi nzima
na kuongeza kuwa huwezi kukamilisha kutaja mafanikio ya vijana bila kutaja SUA katika mchango wake kwa vijana .
Mhe. Abdallah Hamis Ulega (kulia) akimsikiliza Prof. Chibunda wakati alipotembelea maonesho ya Kumbukizi ya Sokoine (Picha zote na Mabula Musa) |
Hayo yamejili
Mei 23, 2023 wakati wa ufunguzi wa Kumbukizi ya miaka 18 ya Hayati Edward Moringe Sokoine mara baada ya Waziri Ulenga
kutembelea maeneo mbalimbali ya chuo ikiwa ni pamoja Hospital ya Taifa ya Rufaa ya Wanyama, Kituo cha Utafiti
na Mafunzo ya Uchumi wa Bluu , Shamba la Malisho ya Mifugo ,mabanda ya maonyesho
pamoja na kushuhudia utiaji saini wa ushirikiano
wa SUA na Taasisi 10 ikiwemo Taasisi
ya Bodi ya Nyama (TMD) na Bodi ya Maziwa.
’’Taifa la Tanzania limepiga
hatua sana toka kupata uhuru kwa sasa kuna nguvu ya watu ya kutosha na ukienda
vyuoni kuna mtaji wa wasomi ambapo kwa
sasa kutokana na Uongozi wa Rais Mama Samia kuwa uongozi unaohitaji matokeo
zaidi hiyo inatoa fursa kwa wataalam wetu
kutekeleza malengo ya kimaendeleo kwa vitendo ili kazi iliyobaki ya uwekezaji wa maarifa yaweze kutafsiriwa na kwenda kukimbizana na
hali ya uchumi wa sasa wa dunia.’’ Amemesema Mhe. Ulega.
Mhe. Abdallah Hamis Ulega akiangalia aina ya malisho ya wanyama yanayofanyiwa utafiti SUA |
Waziri huyo ameongeza kuwa Wizara
inayodhamira ya kufanya kampeni ya kuchanja mifugo nchi nzima kuwa ya lazima ikiwa ni mkakati wa kuwashirikisha vijana
wanaosoma SUA Udaktari wa Mifugo kuanzia mwaka wa tatu wa nne na wa tano
wakishirikiana na wataalam wa maeneo husika na vijana wasio na ajira waliopo mitaani ambapo zoezi hilo la chanjo safari hii
litaratibiwa na Wizara na kupangiwa kalenda ili kulete matokeo chanya kwa kuondosha baadhi
ya magonjwa katika mifugo.
Amesema faida ya kuchanja wanyama
ni kuongeza soko la nyama na kufungua milango
ya uuzwaji wa mifungo kwa uwepo wa soko la uhakika litakalopelekea wafugaji kuvuna na kuchinja nyama nyingi kwa kuvutiwa
na bei nzuri na kutoka kuuza nyama tani elfu 12 pekee kwa
sasa kwenda tani elfu 50 hadi tani laki moja.
‘’Nanaamini wataalam hao wakifanya zoezi hilo
la chanjo kwa vitendo kwa pamoja nchi
zima mpaka vijijini dunia itaona Tanzania imeamua kupambana na magonjwa jambo ambalo litapelekea kuondoa baadhi ya dhana kutoka kwa nchi zinazoogopa nyama ya Tanzania kwa madai ya kuwa na magonjwa kwa kuwa sasa
chanjo itakuwa inaratibiwa siyo ya
kusuasua ’’
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa
Chuo Prof. Rafael Chibunda amesema, pamoja na mafanikio mengi ambayo chuo kimepata tangu kuanzishwa kwake
mwaka 1984 lakini Chuo kilikuwa kinakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na kwamba wanatoa shukurani kwa Rais Samia Hassan Suluhu
kwa kuendelea kutatua changamoto hizo na
kwa mara ya kwanza katika historia ya Chuo SUA kupitia Mradi wa Elimu ya Juu wa
Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) wamepata bilioni 73.6 fedha
hizo tayari zimeanza kugharamia mafunzo, kuboresha miundombinu ya kufundishia na ununuaji wa vifaa mbalimbali chuoni hapo.
Akizungumza kwa upande wa Taaluma
amesema SUA imekuwa na mafanikio ikiwa ni pamoja na
kutajwa na mashirika ya kimataifa kushika nafasi ya pili nchini na nafasi ya 39 kwa ubora Afrika,
ambapo amesema kwenye
kufundisha SUA hakuna maigizo na kwamba mwanafunzi akichagua kusoma SUA amechagua chaguo bora
kabisa na atasoma kwa vitendo na kuwa na
uhakika wa kukubalika katika soko la ajira na hata kujiajiri.
Prof. Chibunda amemuakikishia
Mhe. Ulega kufanya kazi na taasisi walizosaini makubaliano kwa vitendo katika kuongeza wigo wa fursa za ajira kwa vijana kupitia kilimo , mifugo na
uvuvi na kwa kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na pato la taifa kwa
kupitia sekta hiyo kwa kushirikiana kwa pamoja .
Mhe. Abdallah Hamis Ulega kulia akimsikiliza Mganga Mfawidhi wa Hospitali za SUA Dkt. Kasui |
Maonyesho hayo ya kumbukizi ya
sokoine yameanza tarehe 23 Mei, 2023 ambapo yanaambatana na maonyesho ya teknolojia
ya kilimo na ubunifu ambayo yanafanyika katika
viwanja vya SUA, aidha kuna Kongamano la Kisayansi , Huduma za Hospital ya Rufaa
ya Wanyama na Huduma za Hospital za Binadamu ambazo zote ni bure, kauli mbiu
kwa mwaka huu ni ‘Mazingira Wezeshi ya Ushiriki wa Vijana katika Sekta ya Kilimo,
Sera, Miongozo na Utendaji’.
Picha chini Mhe. Ulege akitembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho ya SUA
0 Comments