Na Gladness Mphuru
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Mussa Ali Musa amesema SUA imefanikiwa katika kuhakikisha inawaunganisha wafanyakazi wake na taasisi zingine ikiwemo za kidini kwa matendo yake ikiwemo kuwaalika katika Iftar katika mfungo huu mwezi Mtukufu wa Ramadhan
Akizungumza wa wanajumuiya SUA Aprili 17, 2023 katika ukumbi wa Solomon Mahulangu kwa walioshiriki katika Iftari iliyoandaliwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwasa, amesema hii inaleta faraja kubwa kwa wafanyakazi na wanajuiya wa huo hicho
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda amewasihi watumishi wa chuo hicho kuutumia mwezi mtukufu wa Ramadhan kutenda yaliyo mema, kudumisha umoja na upendo, na kushirikiana kutekeleza majukumu ya chuo bila kujali dini.
Prof. Chibunda ameahidi kuwa uongozi wa SUA utaendelea kujenga mazingira wezeshi kwa ajili ya kuabudu kwa kila mfanyakazi, mwanafuzi na wote waliopo katika jumuiya ya chuo ili kuweza kumuheshimu na kumuabudu mwenyezi Mungu kwa Imani aliyojaaliwa.
Aidha, amewatakia waislamu wote Ramadhan njema na maandalizi mema ya sikukuu ya Eid El Fitr ambayo inatarajiwa kusheherekewa mwishoni mwa wiki hii, na amewakaribisha na kuwashukuru wote waliohudhuria hafla hiyo kwa upendo.
Akizungumza katika Iftari hiyo mwakilishi wa Sheikh wa Mkoa wa Morogoro, amemshukuru Prof. Chibunda kwa kuandaa ibada hiyo ya Iftar na kusema anathamini mualiko huo na anamuomba Mwenyezi Mungu ajalie umoja na ibada ambayo kila mwaka SUA inaandaa Mungu awe mlipaji wa kila jambo.
Iftari hiyo imehudhuriwa Viongozi SUA, Viongozi wa Jumuiya na Taassisi mbalimbali na Wanajumiya ya SUA.
0 Comments