SUAMEDIA

SUA kupatiwa billioni 2.5 kutengeneza mifumo kubaini magonjwa

Na Gladness Mphuru

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia Wakfu wa Utafiti na Udhibiti wa Magonjwa Ambukizi ya Afya moja wa SACIDS, kimepatiwa kiasi cha shilingi billion 2.5 kwaajili ya kutengeneza mifumo ya kuweza kubaini magonjwa mapema punde yanapotokea katika jamii.



Hayo yamebainishwa Machi 23, 2023 na Mmoja wa mwenye Vigoda kumi (10) ambaye ni wa Kwanza kutoka Barani Afrika waliopewa heshima hiyo na Taasisi ya Utafiti ya Afrika Kusini wakishirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania Prof. Gerald Misinzo, katika Kampasi Kuu ya Edward Moringe mjini Morogoro akiwa na wageni kutoka Taasisi ya Utafiti Afrika Kusini walipotembelea Chuoni hapo.

" Tumepewa kiasi cha Billion 2.5 kwa ajili ya kutengeneza mifumo ya kuweza kubaini magonjwa mapema yanapotokea katika jamii, hapo jana Waziri wa Afya alisema kule Bukoba kuna ugonjwa ulitokea ambao uliathiri ndugu zetu na kusababisha vifo vya watu watano na ulisababishwa na ugonjwa wa Marburg na baada ya hapo Serikali imeweza kuzuia ule ugonjwa kuenea ni kwasababu ilishafanya maandalizi mapema", amesema Prof. Misinzo

Prof. Misinzo ameendelea kueleza kwamba wanachokifanya ni kuwezesha Teknolojia za kisasa za kuchambua vinasaba ili kuweza kubaini vihatarishi kwa mapema kabla havijasambaa.

"Utakumbuka kwa mfano Uviko 19 uliposambaa Dunia nzima athari yake ilikuwa kubwa wakati gharama ingekuwa ndogo kama ule ugonjwa ungegundulika mapema na kuzuiwa kusambaa na haifanyiki kwa binadamu pia kwa wanyama" ,amesema Prof. Misinzo

Kwa upande wake Dkt. Dorothy Ngila kutoka Taasisi ya Utafiti ya Afrika Kusini, amesema wamewekeza katika Mpango wa Vigoda vya Utafiti wa Oliver Tambo unaoshikiliwa na Prof. Misinzo hivyo wamekuja kuona ili kujua aina ya utafiti uliofanyika.

Dkt. Ngila amesema pia wamekuja kujua idadi ya wanafunzi wa Shahada za Juu ambao wamekuwa wakipata mafunzo chini ya Kigoda hicho cha Utafiti ili kuwawezesha kuwa wanasayansi bora na kuweza kuisaidia jamii kiuchumi.

Ameongeza kuwa wanategemea Mwenyekiti wa Kigoda hicho ataweza kufanya utafiti wa hali ya juu ambao utasaidia Tanzania na Jumuiya ya Africa Mashariki kiujumla. 




Post a Comment

0 Comments