SUAMEDIA

SUA haitawavumilia wafanyakazi wanaokiuka Maadili ya Utumishi wa Umma - Prof. Chibunda

 

Na, 

Gerald Lwomile

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimesema hakitawavumilia watumishi wote wanaoenda kinyume na Sheria, Kanuni na Taratibu zilizoainishwa kwa watumishi wa Serikali.


Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda akizungumza na watumishi wa SUA hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo (Picha zote na Ayoub Mwigune)

Akizungumza Machi 21, 2023 katika ufunguzi wa mafunzo ya Uthibiti  wa Maadili na Kudhibiti Rushwa yanayotolewa kwa watumishi wa SUA walioajiriwa hivi karibu na wale waliohamia katika Chuo hicho,  Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda amesema kinayachulia mafunzo hayo kwa umuhimu mkubwa kwani ni kutekeleza agizo la Serikali Kuu.

Prof. Chibunda amesema SUA itawachukulia hatua kali kwa mujibu wa kanuni na sheria za utumishi wa umma watumishi wote ambao watakiuka kwa makusudi na hata kwa uzembe katika utekelezaji wa majumu yao.

“Sisi kama Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo tunatilia maanani na umuhimu wa pekee kwa wafanyakazi wetu kuweza kufahamu taratibu zote ambazo zinatelekezwa na sheria mbali za Serikali kuhusu uadilifu katika utumishi wa umma na kupiga vita rushwa katika Taasisi yetu na Serikali kwa ujumla” amesema Prof. Chibunda


Wafanyakazi wa SUA pichani wakifuatilia mafunzo kutoka kwa wawezeshaji

Awali akizungumza kabla ya Mgeni Rasmi Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam Prof. Maulid Mwatawala amewataka watumishi hao kuhakikisha wanaujua utamaduni wa Taasisi wanayoifanyia kazi yaani SUA.

Amesema watumishi wengi wamekuwa hawajui tamaduni ya Taasisi jambo ambalo limekuwa likileta mchanganyiko katika utendaji wa kazi, aidha amewataka watumishi hao kuacha tamaa katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuepuka rushwa.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kuthibiti Uadilifu (KKU) SUA Prof. Christopher Mahonge amesema uongozi wa juu wa Taasisi hiyo umekuwa ukiunga mkono jitihada za Kamati hiyo jambo linaloweza kuzaa matunda mazuri ya kuwa na watumishi wenye uadilifu na wasiopokea rushwa.



Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda waliokaa (katikati),  kushoto aliyekaa ni Mwenyekiti wa KKU Prof. Mahonge 




Post a Comment

0 Comments