Na: Amina Hezron - Njombe
Watafiti wa Mradi wa GRILI uliohusisha uvumbuzi na utengenezaji wa mwongozo wa kibiashara wa bidhaa za mimea dawa wametakiwa kuwasilisha mapendekezo ya kisera ya utafiti huo Serikalini ili biashara hiyo iingie katika mfumo rasmi na hivyo kuchangia pato la Jamii na Taifa.
1. Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omary ambae alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa Mhe. Antony Mtaka katika Kongamano la kisera la wadau wa mnyororo wa thamani wa mimea dawa akifungua Kongamano hilo.
“Ukamilifu na utekelezaji wa Ajenda 2030 hasa
katika nchi zinazoendelea unategemea sana uwekezaji katika tafiti za kisayansi,
Teknolojia, Ubunifu na Uvumbuzi kwa kuzingatia mahitaji yetu kwa uhalisia wake”,
alisema Judica.
Aidha
ameeleza kuwa Serikali imeazimia na kujitolea kuwezesha mtafiti mmoja mmoja na
Taasisi mbalimbali kutafiti, kubuni, na kuboresha teknolojia katika sekta zote
za kiuchumi ikiwemo sekta ya Viwanda ambayo kwa sasa inakua kwa kasi kubwa
hivyo ametoa rai kwa watafiti kuendelea kufanya tafiti ambazo zitaibua ubunifu
katika maendeleo ya sekta mbalimbali.
Awali
akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua kongamano hilo Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Upande wa Taaluma,
Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Walad Mwatawala amesema zaidi ya
asilimia 80 ya watanzania wanatumia dawa za asili zitokanazo na mimea kwa ajili
ya afya na kujikimu kwa kipato.
“Zaidi
ya yote, wadau wengine tayari wanasafirisha nje ya nchi mazao au sehemu za
mimea hiyo kama biashara na kujipatia kipato na kuimarisha uchumi wao , soko la
kimataifa la bidhaa za rasilimali za kijani (GRPs), ikiwa ni pamoja na dawa za
asili, ni zaidi ya Dola za kimarekani bilioni 170 na linaendelea kukua kwa
asilimia 15 kwa mwaka, huku kukiwa na shauku kubwa ya bidhaa mpya kutoka
Afrika”, alisema Prof Mwatawala.
Akizungumzia
yaliyofanyika kupitia mradi huo Mkuu wa Mradi kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo SUA Prof. Faith Mabiki amesema kuwa utafiti huo umeweza kutambulisha
mnyororo wa thamani na kugundua wadau muhimu ambao wakishirikiana wanaweza
kusaidia kuinua sekta ya mazao ya kijani hasa tiba asili kwenda kuchangia
katika pato la Taifa na mtu mmoja mmoja.
“Kwahiyo
wadau waliopo hapa wengi wanajiona katika mnyororo wa thamani huu na huu
tumeutengenezea chapisho maalumu ambalo limetoka katika ulimwengu lakini pia
tumeweza kutengeneza muundo wa kibiashara”, alisema Prof Mabiki.
Akitoa
neno la shukrani kwa mgeni rasmi Mkurugenzi,Kurugenzi ya Shahada za
Uzamili,Utafiti na Uhaulishaji wa Teknolojia kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo Prof. Esron Karimuribo amesema kuwa anashukuru kwa ahadi za Serikali katika
kuendelea kutumia matokeo ya tafiti ambazo zinasaidia katika kuandaa au
kuboresha sera lakini pia maendeleo ya Taifa.
“Tunafarijika
sana kama watafiti tukiona tunafanya kazi ambayo inaweza ikathaminiwa katika
kutoa mchango kwa taifa tunashukuru sana, lakini umetuahidi serikali itakuwa na
watafiti bega kwa bega katika shughuri zetu ikiwa ni pamoja na habari ya kuongeza fedha na
bajeti ya utafiti, kwetu sisi tupo tayari kwasababu tuna ujuzi na rasilimali
fedha inapopatikana tunakuahidi tutatoa mchango wetu katika kutoa majawabu
ambayo yanalikabili taifa na jamii “, alisema Prof. Karimuribo.
1. Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Walad Mwatawala akitoa salamu za SUA kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua Kongamano hilo.
1. Mkurugenzi,Kurugenzi ya Shahada za Uzamili,Utafiti na Uhaulishaji wa Teknolojia kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Esron Karimuribo akitoa neon la shukrani kwa mgeni rasmi.
0 Comments