SUAMEDIA

Watafiti wa Mradi wa FoodLAND wafanya utafiti wa vifungashio bora vya vyakula

Na: Amina Hezron  - Zanzibar

Kutokana na katazo la serikali juu ya matumizi ya vifungashio vya plastiki nchini Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kupitia Mradi wa Chakula Kilimo na Lishe (FoodLAND) wameanzisha teknolojia ya utengenezaji wa vifungashio kwakutumia maganda ya Nanasi ambavyo vitasaidia katika uhifadhi wa vyakula.

Mkuu wa Mradi wa Chakula Kilimo na Lishe (FoodLAND) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Susan Mchimbi Msolla.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mradi wa Chakula Kilimo na Lishe (FoodLAND) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Susan Mchimbi Msolla alipokuwa akizungumza na SUAMEDIA wakati wa Mkutano Mkuu wa tatu wa Mwaka wa Mradi huo Visiwani Zanzibar.

 Amesema kutokana na katazo hilo mradi ukaona ni vyema wao kama watafiti kuangalia namna ya kutengeneza vifungashio kwakutumia malighafi za nchini ambavyo vitatumika pia kuhifadhia bidhaa ambazo zinatengenezwa katika mradi.

“Haya maganda ya Nanasi yanaweza kutumiwa kutengeneza na kutoa vifungashio vizuri tu ambavyo sisi katika mradi wetu hivyo vifungashio tutatumia kufungashia Unga wa lishe tuonaotengeneza kwaajili ya kulisha watoto na watu wazima lakini pia tunaweza tukatumia katika kufungashia samaki ambao watakuwa wanazalishwa kupitia mradi wetu unaotekelezwa Wilayani Kilombero”, alisema Prof. Nchimbi.

Akizungumzia teknolojia hiyo Mtafiti anayesimamia mambo ya kusaga katika mradi huo kutoka SUA Dkt. Rashid Suleiman ameleza kuwa mpaka sasa teknolojia hiyo imekamilika kwa asilimia sabini na mpaka mwisho wa mwezi huu au mwezi ujao sampuli ya kwanza inategemewa kuwa tayari imeshamalizika kutengenezwa na kujaribiwa katika matumizi.

Mtafiti anayesimamia mambo ya kusaga katika mradi huo kutoka SUA Dkt. Rashid Suleiman.

Dkt Suleiman ameeleza wakati wa utekelezaji wa tafiti katika eneo Kilombero mkoni Morogoro wamebaini uwepo wa changamoto ya utapia mlo hivyo watatoa elimu kwa wajasiliamali hasa wanawake namna ya kukausha mboga za majani na kuweza kutumia pamoja na kukausha samaki aina ya Sangara na Kambale.

“Kwenye mradi tunahusika pia kuwasaidia watu kuhifadhi mazao yao ili yakae muda mrefu na hapo kwasababu tunazalisha maharage kwenye huu mradi kwahiyo tulikuwa  tunataka tuwasaide watu wa Mvomero kuhifadhi maharage yao kwa muda mrefu vilevile tuna kitu kinaitwa smart storage ambapo sisi pia kwakushirikina na nchi zingine tano tutakuja na njia mbadala ya kuhifadhi maharage mabichi kukaa muda mrefu kwakuwa yanathamani zaidi yakiuzwa mabichi na yanaweza kukaa kwa muda mrefu”, alisema Dkt Suleimani.


 

Post a Comment

0 Comments