SUAMEDIA

Bilioni 18 za Mradi wa HEET kuboresha Miundombinu ya Kampasi ya SUA Mizengo Pinda

 Na: Calvin Gwabara – Katavi.

Uongozi wa Kampasi ya SUA ya Mizengo Pinda Mkoani Katavi umeishukuru Serikali kwa kuwezesha kupatikana kwa fedha zaidi ya shilingi biloni 18 kupitia mradi Mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi (HEET) ambazo zinakwenda kuboresha miundombinu cha Kampasi hiyo kuwa ya kisasa.

Rasi wa Ndaki hiyo Prof. Josiah Katani wakati akiongea na SUAMEDIA kuhusu utekelezaji wa mradi wa HEET kwenya kampasi hiyo.

Shukrani hizo zimetolewa na Ras wa Ndaki hiyo Prof. Josiah Katani wakati akiongea na SUAMEDIA kuhusu mikakati na mipango iliyowekwa kupitia mradi huo kwenye kuboresha miundombinu za kampasi hiyo mpya ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo iliyopo Kata ya kibaoni Halmashauri ya Mpimbwe Mkoani Katavi.

“Kwakweli tunaendelea kuishurku serikali kwa kutupatia dola za kimarekani milioni nane kutoka na mradi huu wa HEET,kwetu imekuwa ni furaha kwa sababu tunakwenda kufungua chuo chetu kiweze kukua kwa kuwekea miundombinu ambayo ni muhimu, katika fedha hizo ambazo ni sawa na shilingi bilioni 18 zitajenga hosteli ya wanafunzi yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 600, jengo la Mtambuka ambalo litakuwa na madarasa na maabara litakalobeba wanafunzo 2500 hadi 3000, kujenga bwalo la Chakula la watu 300 kwa mara moja pamoja na ununuzi wa Basi la kubebea Wnafunzi ” alisema Prof. Katani.

Rasi huyo wa Ndaki amesema pamoja na majengo hayo pia Mradi huo wa HEET pia utaboresha na kutengeneza shamba la mafunzo (Model Farm) pamoja na shamba la nyuki na kwamba jitihada hizo zote ni kuwezesha wanafunzi wa Kampasi hiyo kufanya mafunzo kwa vitendo kitu ambacho ni muhimu katika kupata wataalamu waliobobea kwenye fani hizo.

Muonekano wa Mbele kuingia jengo la Utawala la Kampasi ya Mizengo Pinda Mkoani Katavi

Prof. Katani amesema kukamilika kwa mejengo na miundombinu hiyo kutaifanya kampasi hiyo na Chuo kukua zaidi na kuvutia wanafunzi wengi kusoma kwenye kampasi ya Mizengo Pinda kwakuwa itakuwa na vitu vyote muhimu vinavyohitajika kwa mwanafunzi kujifunza.

Aidha Rasi wa Ndaki hiyo amepongeza pia mradi huo kwa kutoa ufadhili kwa Wanataaluma wake kwenda kusoma kwakuwa wengi walikuwa wakufunzi lakini baada ya kurudi masomoni wakiwa na Shahada ya Uzamili watakuwa Wahadhiri wasaidizi.

“Hawa walimu watakapotoka masomoni sasa watakuwa na uwezo wa kufundisha zile kozi za shahada ya kwanza lakini pia stashahada na astashahada kwahiyo sisi kama Chuo tunaona ni mafanikio makubwa sana kwetu yanayoletwa na mradi huu wa HEET”alifafanua Prof. Katani.

Prof. Katani amesema wanapongeza pia Chuo kwa namna wanavyotekeleza mradi huo kwa ushirikishwaji mkubwa lakini pia umekuwa ukitoa mafunzo katika Nyanja mbalimbali kwani wameshapokea timu mbalimbali zinazokuja kuchukua maoni ya utekelezaji lakini pia nyingine kutoa mafunzo kuhusu masuala ya Jinsia.

Amesema ni mradi wa aina yake ambao umegusa kila sehemu mfano kujengea uwezo Wanataaluma na Wanafunzi lakini pia kuwawekea miundombinu ambayo itawezesha ufunishaji kuwa mwepesi pamoja na kuboresha huduma za mtando ambazo ni muhimu katika ufundishaji na kujifunza.

Post a Comment

0 Comments