Na: Amina Hezron - Zanzibar
Kutokana na katazo la serikali
juu ya matumizi ya vifungashio vya plastiki nchini Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo SUA kupitia Mradi wa Chakula Kilimo na Lishe (FoodLAND) wameanzisha
teknolojia ya utengenezaji wa vifungashio kwakutumia maganda ya Nanasi ambavyo
vitasaidia katika uhifadhi wa vyakula.
Mkuu wa Mradi wa Chakula Kilimo na Lishe (FoodLAND) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Susan Mchimbi Msolla. |
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mradi
wa Chakula Kilimo na Lishe (FoodLAND) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof.
Susan Mchimbi Msolla alipokuwa akizungumza na SUAMEDIA wakati wa Mkutano Mkuu
wa tatu wa Mwaka wa Mradi huo Visiwani Zanzibar.
Amesema kutokana na katazo hilo mradi ukaona ni
vyema wao kama watafiti kuangalia namna ya kutengeneza vifungashio kwakutumia
malighafi za nchini ambavyo vitatumika pia kuhifadhia bidhaa ambazo
zinatengenezwa katika mradi.
“Haya maganda ya Nanasi yanaweza
kutumiwa kutengeneza na kutoa vifungashio vizuri tu ambavyo sisi katika mradi
wetu hivyo vifungashio tutatumia kufungashia Unga wa lishe tuonaotengeneza
kwaajili ya kulisha watoto na watu wazima lakini pia tunaweza tukatumia katika
kufungashia samaki ambao watakuwa wanazalishwa kupitia mradi wetu unaotekelezwa
Wilayani Kilombero”, alisema Prof. Nchimbi.
Akizungumzia teknolojia hiyo
Mtafiti anayesimamia mambo ya kusaga katika mradi huo kutoka SUA Dkt. Rashid
Suleiman ameleza kuwa mpaka sasa teknolojia hiyo imekamilika kwa asilimia
sabini na mpaka mwisho wa mwezi huu au mwezi ujao sampuli ya kwanza inategemewa
kuwa tayari imeshamalizika kutengenezwa na kujaribiwa katika matumizi.
Mtafiti anayesimamia mambo ya kusaga katika mradi huo kutoka SUA Dkt. Rashid Suleiman. |
Dkt
Suleiman ameeleza wakati wa utekelezaji wa tafiti katika eneo Kilombero mkoni
Morogoro wamebaini uwepo wa changamoto ya utapia mlo hivyo watatoa elimu kwa
wajasiliamali hasa wanawake namna ya kukausha mboga za majani na kuweza kutumia
pamoja na kukausha samaki aina ya Sangara na Kambale.
“Kwenye
mradi tunahusika pia kuwasaidia watu kuhifadhi mazao yao ili yakae muda mrefu
na hapo kwasababu tunazalisha maharage kwenye huu mradi kwahiyo tulikuwa tunataka tuwasaide watu wa Mvomero kuhifadhi
maharage yao kwa muda mrefu vilevile tuna kitu kinaitwa smart storage ambapo sisi
pia kwakushirikina na nchi zingine tano tutakuja na njia mbadala ya kuhifadhi
maharage mabichi kukaa muda mrefu kwakuwa yanathamani zaidi yakiuzwa mabichi na
yanaweza kukaa kwa muda mrefu”, alisema Dkt Suleimani.
0 Comments