Na: Calvin Gwabara – Katavi.
Uongozi
wa Kampasi ya SUA ya Mizengo Pinda Mkoani Katavi umeishukuru Serikali kwa
kuwezesha kupatikana kwa fedha zaidi ya shilingi biloni 18 kupitia mradi Mradi
wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi (HEET) ambazo zinakwenda kuboresha
miundombinu cha Kampasi hiyo kuwa ya kisasa.
Shukrani
hizo zimetolewa na Ras wa Ndaki hiyo Prof. Josiah Katani wakati akiongea na
SUAMEDIA kuhusu mikakati na mipango iliyowekwa kupitia mradi huo kwenye
kuboresha miundombinu za kampasi hiyo mpya ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
iliyopo Kata ya kibaoni Halmashauri ya Mpimbwe Mkoani Katavi.
“Kwakweli
tunaendelea kuishurku serikali kwa kutupatia dola za kimarekani milioni nane
kutoka na mradi huu wa HEET,kwetu imekuwa ni furaha kwa sababu tunakwenda
kufungua chuo chetu kiweze kukua kwa kuwekea miundombinu ambayo ni muhimu,
katika fedha hizo ambazo ni sawa na shilingi bilioni 18 zitajenga hosteli ya wanafunzi
yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 600, jengo la Mtambuka ambalo litakuwa na
madarasa na maabara litakalobeba wanafunzo 2500 hadi 3000, kujenga bwalo la
Chakula la watu 300 kwa mara moja pamoja na ununuzi wa Basi la kubebea Wnafunzi
” alisema Prof. Katani.
Rasi huyo
wa Ndaki amesema pamoja na majengo hayo pia Mradi huo wa HEET pia utaboresha na
kutengeneza shamba la mafunzo (Model Farm) pamoja na shamba la nyuki na kwamba
jitihada hizo zote ni kuwezesha wanafunzi wa Kampasi hiyo kufanya mafunzo kwa
vitendo kitu ambacho ni muhimu katika kupata wataalamu waliobobea kwenye fani
hizo.
Muonekano wa Mbele kuingia jengo la Utawala la Kampasi ya Mizengo Pinda Mkoani Katavi |
Prof.
Katani amesema kukamilika kwa mejengo na miundombinu hiyo kutaifanya kampasi
hiyo na Chuo kukua zaidi na kuvutia wanafunzi wengi kusoma kwenye kampasi ya
Mizengo Pinda kwakuwa itakuwa na vitu vyote muhimu vinavyohitajika kwa
mwanafunzi kujifunza.
Aidha
Rasi wa Ndaki hiyo amepongeza pia mradi huo kwa kutoa ufadhili kwa Wanataaluma
wake kwenda kusoma kwakuwa wengi walikuwa wakufunzi lakini baada ya kurudi
masomoni wakiwa na Shahada ya Uzamili watakuwa Wahadhiri wasaidizi.
“Hawa
walimu watakapotoka masomoni sasa watakuwa na uwezo wa kufundisha zile kozi za
shahada ya kwanza lakini pia stashahada na astashahada kwahiyo sisi kama Chuo
tunaona ni mafanikio makubwa sana kwetu yanayoletwa na mradi huu wa HEET”alifafanua
Prof. Katani.
Prof.
Katani amesema wanapongeza pia Chuo kwa namna wanavyotekeleza mradi huo kwa
ushirikishwaji mkubwa lakini pia umekuwa ukitoa mafunzo katika Nyanja mbalimbali
kwani wameshapokea timu mbalimbali zinazokuja kuchukua maoni ya utekelezaji
lakini pia nyingine kutoa mafunzo kuhusu masuala ya Jinsia.
Amesema
ni mradi wa aina yake ambao umegusa kila sehemu mfano kujengea uwezo Wanataaluma
na Wanafunzi lakini pia kuwawekea miundombinu ambayo itawezesha ufunishaji kuwa
mwepesi pamoja na kuboresha huduma za mtando ambazo ni muhimu katika
ufundishaji na kujifunza.
0 Comments