Na: Siwema , Hanipher Mkamba.
Wanafunzi wa Shule za Sekondari nchini washauriwa kufanya ziara za kimafunzo yatakayopelekea kuwa bora kielimu na kujifunza mbinu za kimaisha katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mkoani Morogoro kutokana na elimu itolewayo inalenga moja kwa moja maisha ya sasa na ya baadae kwa wanafunzi hao.
Hayo wamesemwa na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Ruvu Emmanuel Mgode mara baada ya kuwasili SUA kwa ziara na kutumia fursa hiyo kuonesha wanafunzi wa shule yake kuwa SUA ni mahala sahihi kwa mwanafunzi kujifunza kwa vitendo na kwa ziara hiyo itawasaidia kuwa bora kutokana na mafunzo kwa nadharia kwani itakuwa chachu ya kuendeleza miradi waliyoanzisha katika shule yao.
Nao baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita kutoka Shule hiyo Agape Sarakiky na Neema Alule wamesema kuwa wamejifunza vitu vingi kuhusu kilimo na kutolea mfano namna ambavyo wanaweza kuanzisha bustani za maua na matunda amabayo inaweza kuwasaidia baadae hata kama wakikosa ajira ya kudumu na kuongeza kuwa kwa sasa wataweza kutumia rasilimali zinazopatikana karibu yao kama fursa mfano maji kwa kutengeneza Bwawa la Samaki ili kujikimu kimaisha.
Aidha, wameongeza kuwa mafunzo waliyopata yatawasaidia katika masomo yao kujibu mitihani pia kupambana na ukosefu wa ajira hivyo watatumia mafunzo hayo kama fursa kujiajiri na kuwaasa wanafunzi wanapopata fursa ya namna hiyo kutopuuzia mambo muhimu waliyojifunza badala yake wayatumie kama nafasi ya kutengeneza maisha yao.
“ Tusirelax na tusitegemee ajira sana kutoka serikalini kwa hiyo tunatakiwa kujiajiri na huku tukikumbuka kuwa Tanzania yetu ni ya viwanda hivyo inahitaji kujitoa ili kuendeleza viwanda hivyo tukizingatia kuwa hata shuleni kwetu tunalima mbogamboga na tunayo mabwawa ya samaki kwa hiyo mara baada ya kufika shule tutaendeleza zaidi kutokana na elimu tuliyopata.” Amesema Agape Sarakiky.
PICHA NA GOJO MOHAMED
0 Comments