SUAMEDIA

Uraibu wa madawa ya kulevya kwa vijana kusababisha kina mama wengi kuumia na kupata magonjwa kama Moyo na Vidonda vya Tumbo

Na Editha Mloli

Uraibu wa madawa ya kulevya kwa vijana ambao unapelekea vijana wengi kupoteza uhalisia wao wa kawaida umeonekana kusababisha kina mama wengi kuumia na kupata magonjwa ikiwa ni pamoja na magonjwa ya Moyo na Vidonda vya Tumbo 



Hayo yamesemwa na  Meneja wa Kituo cha Kuwasaidia Vijana walioathirika na madawa ya kulevya kinachofahamika kwa jina la Free at Last Soba House na Katibu wa Jumuiya ya Vijana wanaopata nafuu Tanzania Conerstone Recovery Community Michael Mlowe wakati akizungumza na SUAMEDIA. 

Mlowe amesema wamama wengi wamekuwa wakitumia muda mwingi kuwawaza watoto wao ambapo pia amewaomba wanaharakati pamoja na wanasaikolojia mbalimbali kujaribu kujikita katika kuwasaidia wakina mama wenye watoto wanaotumia madawa ya kulevya ili kuokoa kinamama ambao wakati mwingine wanapoteza maisha yao kwa ajili

Amesema  kipindi vijana hawa wanapotumia madawa haya ya kulevya hawaoni tatizo lolote na kuona kila anachokifanya ni sahihi kwa upande wake kwa kuwa wanatumia madawa haya ili waishi ambapo kwa upande wa wazazi hususani mama yeye huumia kuliko hata kijana wake kwa wakati huo.

“Kipindi kile anakuwa anatumia madawa haya ya kulevya hususani Heroin anakuwa anateseka ila haumii ila mama ndo anaumia kwa sababu nimekutana na kesi ambazo kina mama wanapata magonjwa kama BP, mara Vidonda vya tumbo, wengine wanaogopa kujichanganya katika masuala ya kijamiikwa sabau tu ya aibu ya watoto wao lakini pia wengine wanapoteza maisha.

Mlowe amesema jamii inapaswa kuwasidia vijana kuondokana na matumizi haya ya dawa za kulevya na kutokuwanyanyapa bali kuwapeleka katika sehemu ambazo zinabadilisha tabia zao ili pia kuwasaidia kina mama wenye vijana wahanga wa madawa ya kulevya na kuokoa taifa la Tanzania kwa ujumla.



Post a Comment

0 Comments