Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) leo Septemba 5,
2022 ameitambulisha rasmi kwa Bodi na Menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) timu itakayofanya mapitio ya utaratibu wa
utoaji mikopo kwa miaka mitano iliyopita ili kuona namna ya kuboresho
utaratibu huo.
Amefanya utambulisho huo jijini Dar
es Salaam ambapo ameongeza kuwa timu hiyo pia itaangalia taarifa ambazo
zimekuwa zikitumika kuomba mikopo kwa kipindi hicho ili kuona iwapo
zinatosheleza au kutahitajika taarifa za ziada ili kuboresha zoezi hilo na
kuipa timu hiyo mwezi mmoja kukamilisha kazi hiyo.
Profesa Mkenda amewataja wajumbe wa
timu hiyo kuwa ni Prof. Allen Mushi, Dkt. Martin Chegere na Iddi Makame na
kuongeza kuwa wajumbe hao wote ni wataalamu ambao ana imani kuwa watafanya kazi
kwa weledi na umakini wa hali ya juu.
"Lengo kuu la kufanya mapitio
haya ni kuhakikisha tunaboresha zoezi la utoaji mikopo na kuhakikisha inatolewa
kwa haki na kufuata vigezo vilivyotangazwa ili kupunguza au kumaliza kabisa
malalamiko ambayo yamekuwa yakijitokeza," amefafanua Prof. Mkenda.
0 Comments