NA: Winfrida Nicolaus
Wananchi wametakiwa
kufika kwenye Maonesho ya 29 ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi Kanda ya Mashariki
katika Banda la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Kitengo cha Bustani kwaajili
ya kupata huduma za namna bora ya kulima Kilimo cha Kisasa chenye tija cha muda
mfupi.
Amebainisha hayo
Msimamizi wa Kitengo cha Bustani katika Ndaki ya Kilimo SUA Bw. Roman Michael
Mfinanga wakati akizungumza na SUAMEDIA kuhusiana na vitu ambavyo wanaionesha
jamii katika Maonesho hayo yanayofanyika Mkoani Morogoro.
Amesema Kitengo cha
Bustani kinajihusisha na Uzalishaji wa Matunda ya aina tofauti, Maua, Viungo
pamoja na Mboga mboga vilevile kinahusika na Tafiti mbalimbali kuhusiana na
Matunda, Mbogamboga pamoja na Viungo ambapo zinawafikia wananchi kwa namna ya
kupata huduma ambazo ni pamoja na kuwawezesha kuzalisha Matunda kwa muda mfupi
ambayo yanaweza kutumika kwaajili ya kuboresha afya katika miili yao.
Bw. Mfinanga amesema kitengo
hicho cha Bustani kinahusika pia katika uzalishaji wa Mazao ya Bustani ambayo
yanaweza kulimwa katika maeneo mengi ya Tanzania na kuwa na ubora mkubwa
kwakuwa yanafuata taratibu zote za Kilimo cha Kisasa, kilimo ambacho kitawawesha
wananchi kujiongezea kipato na kuweza kuzihudumia familia zao ikiwa ni pamoja
na kusomesha Watoto wao.
“Tunawashauri wananchi
kufika kwenye Maonesho ya 8-8 katika Banda la SUA Kitengo cha Bustani kwaajili
ya kupata huduma za namna bora ya kufanya Kilimo cha Kisasa cha muda mfupi na
cha Tija kwenye maisha yao ya kila siku na inapokea Wanafunzi wa Shahada
mbalimbali, hivyo tunawasisitiza kufika kwenye Viwaja hivi vya Mwalimu Julius
Nyerere kuelekezwa namna ya kujiunga na kozi zinazotolewa kwa manufaa yao”, amesema
Mfinanga.
Aidha amesema katika Maonesho
hayo wanayo Matunda ya aina mbalimbali kwa maana ya Miembe aina nne, Parachichi
aina tatu, Jamii ya Michungwa aina sita, Mipera ya kisasa rangi nyekundu, Yellow
Passion na Pupple Passion za kutosha ambazo zimelimwa kitaalam
kabisa kwaajili ya kulinda Afya ya mtumiaji.
0 Comments