NA:Winfrida Nicolaus
Wakulima pamoja na watu
wanaohitaji kuingia katika shughuli za Kilimo wametakiwa kutembelea banda la
SUA katika Idara ya Sayansi ya Udongo na Jiolojia kwenye Maonesho ya 29
yaWakulima, Wafugaji na Wavuvi kanda ya Mashariki yanayofanyika mkoani Morogoro
ili kupima Sampuli zao za Udongo kwaajili ya Kilimo chenye Tija na Endelevu.
![]() |
| Mtaalam wa Udongo Bw. Louis Mdoe kutoka Ndaki ya Kilimo, Idara ya Sayansi ya Udongo na Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wakati akizungumza kuhusu umuhimu wa kupima udongo kabla ya kuanza kulima. |
Amesema hayo Mtaalam wa Udongo
Bw. Louis Mdoe kutoka Ndaki ya Kilimo, Idara ya
Sayansi ya Udongo na Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA
wakati akizungumza Mubashara na SUA FM kutoka kwenye viwanja vya Maonesho hayo.
Amesema kuna umuhimu
mkubwa kwa Wakulima kujua vipimo vya Udongo kwa kuwa vinawasaidia kutambua aina
ya zao kwenye Udongo husika vilevile aina ya Virutubisho katika shamba lake kwa
mazao husika na kwamba hiyo inapelekea mkulima kuwa na kilimo cha uhakika na
cha tija.
Bw. Mdoe amesema kuna
Virutubisho kama Salfa, Nitrojeni, Potasium, Calsium pamoja na Magnesium yapo
baadhi ya mazao ambayo yanapendelea hivyo Virutubisho hivyo unapokuwa umepima
Udongo wako unaweza ukajua ni aina gani ya zao unaweza ukalipanda katika shamba
lako ili kujipatia Tija kwenye mavuno yako.
“Kwa mfano ukachukua
sampuli ya udongo wako halafu ukajua udongo wako huo una kiasi kikubwa cha
mfinyanzi na tunafahamu kuwa udongo huo wa mfinyanzi unatabia ya kukwamisha
maji kwa kiasi kikubwa kwa hiyo ni vizuri ukachagua zao ambalo linahitaji eneo
la kutuamisha maji ambalo ni Mpunga”, amesema Mdoe.
Aidha amesema kama Mkulima
anahitaji kuchukua Sampuli ya Udongo katika shamba lake ni muhimu kumtumia Mtaalam
ambaye anaweza kuchukua sampuli hiyo kitaalam kwasababu sampuli yoyote ile ya
udongo inauwakilishi kulingani na ukubwa wa eneo la shamba lako.
“Kwa mfano sampuli ya
Udongo inayowakilisha kiasi cha Tani 20,000 kwa Ekali Moja katika Tani hizo 20,000
unaweza ukaleta Udongo wa Kilo Moja na ndio uwakilishi husika kwa hiyo unatakiwa
uchukue sampuli yako kama una Elimu ya Sayansi ya Kilimo na si mtu yoyote yule
kwasababu anaweza kuleta Sampuli ambayo si wakilishi kwa eneo husika”, amesema Mtaalam
huyo.


0 Comments