SUAMEDIA

Wananchi wamehamasishwa kufika katika Banda la SUA ktk maonesho ya 88 yanayoendelea

 

NA: Winfrida Nicolaus

Wananchi wametakiwa kufika kwenye Maonesho ya 29 ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi Kanda ya Mashariki katika Banda la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Kitengo cha Bustani kwaajili ya kupata huduma za namna bora ya kulima Kilimo cha Kisasa chenye tija cha muda mfupi.










Amebainisha hayo Msimamizi wa Kitengo cha Bustani katika Ndaki ya Kilimo SUA Bw. Roman Michael Mfinanga wakati akizungumza na SUAMEDIA kuhusiana na vitu ambavyo wanaionesha jamii katika Maonesho hayo yanayofanyika Mkoani Morogoro.

Amesema Kitengo cha Bustani kinajihusisha na Uzalishaji wa Matunda ya aina tofauti, Maua, Viungo pamoja na Mboga mboga vilevile kinahusika na Tafiti mbalimbali kuhusiana na Matunda, Mbogamboga pamoja na Viungo ambapo zinawafikia wananchi kwa namna ya kupata huduma ambazo ni pamoja na kuwawezesha kuzalisha Matunda kwa muda mfupi ambayo yanaweza kutumika kwaajili ya kuboresha afya katika miili yao.

Bw. Mfinanga amesema kitengo hicho cha Bustani kinahusika pia katika uzalishaji wa Mazao ya Bustani ambayo yanaweza kulimwa katika maeneo mengi ya Tanzania na kuwa na ubora mkubwa kwakuwa yanafuata taratibu zote za Kilimo cha Kisasa, kilimo ambacho kitawawesha wananchi kujiongezea kipato na kuweza kuzihudumia familia zao ikiwa ni pamoja na  kusomesha Watoto wao.

“Tunawashauri wananchi kufika kwenye Maonesho ya 8-8 katika Banda la SUA Kitengo cha Bustani kwaajili ya kupata huduma za namna bora ya kufanya Kilimo cha Kisasa cha muda mfupi na cha Tija kwenye maisha yao ya kila siku na inapokea Wanafunzi wa Shahada mbalimbali, hivyo tunawasisitiza kufika kwenye Viwaja hivi vya Mwalimu Julius Nyerere kuelekezwa namna ya kujiunga na kozi zinazotolewa kwa manufaa yao”, amesema Mfinanga.

Aidha amesema katika Maonesho hayo wanayo Matunda ya aina mbalimbali kwa maana ya Miembe aina nne, Parachichi aina tatu, Jamii ya Michungwa aina sita, Mipera ya kisasa rangi nyekundu, Yellow Passion na Pupple Passion za kutosha ambazo zimelimwa kitaalam kabisa kwaajili ya kulinda Afya ya mtumiaji.


 

Post a Comment

0 Comments