SUAMEDIA

Wakulima wapata Fursa kujifunza namna ya kubadilisha mazao ya Shamba kuwa bidhaa zenye thamani kibiashara

 NA:Winfrida Nicolaus

Idara ya Teknolojia ya Chakula na Uchakataji wa Mazao ya Shambani iliyopo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA inatoa Elimu ya namna ya kubadilisha mazao ya shamba kuwa katika bidhaa zenye thamani kibiashara na hivyo kuwawezesha wakulima kukua uchumi.




Ameelezea  hayo Fundi Sanifu Maabara kutoka Idara hiyo Bw. Tamambele Masinga wakati akizungumza na SUAMEDIA kwenye Maonesho ya 29 ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi Kanda ya Mashariki yanayofanyika mkoani Morogoro.

Amesema kile wanachofanya ni kujaribu kubadilisha Mazao ya Shamba kuwa katika Bidhaa bora hivyo wanayaongezea thamani mazao hayo ili yaweze kuwa na muda mrefu ambapo Mwanafunzi anajifunza kutazama mazao ya Shamba katika bidhaa tofauti tofauti za kibiashara na kuweza kujikwamua kiuchumi.

Bw. Masinga amesema anawahamasisha wananchi kupitia Mafunzo mbalimbali ya muda mfupi kwa faida yao wenyewe kwasababu wale ambao wanapata ujuzi kama wa Uchakataji wa Mazao kama vile Matunda kwaajili ya Juice, Vinegar pamoja na Wine au Usindikaji wa Mbogamboga watasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uharibifu wa Mazao ya Shamba ambayo yangeweza kuharibika kama yangeachwa bila kubadilishwa au kuyaongezea thamani.

Aidha amesema vitu ambavyo wanafunzi wameweza kufanikiwa kuvitengeneza kupitia usimamizi mzuri wa Wataalam wa Maabara na wanavionesha katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki kwa mwaka huu wa 2022 ni pamoja na Chili source ambayo imetokana na Karoti, na Nyanya, Tomato Source pamoja na Mkate uliotengenezwa kwa Unga wa Viazi Lishe, Maharage ya Soya na Ngano ambayo haijakobolewa.

“Hivyo vitu ambavyo tumekuja kuhamasisha Wananchi ni kuwashauri kupitia short course au Mafunzo ya muda mfupi wakaweze kujifunza vizuri Zaidi mfano tunafanya uchakataji wa Matunda ambapo tunatengeneza Juice, Charm, Vinega pamoja na Wine kwa hiyo ni vitu ambavyo tunajifunza mbali na hapo pia tunafanya usindikaji wa mbogamboga”, amesema Bw. Masinga

“Na hapa tumekuja na chili souce ambayo imetengenezwa kwa karoti, nyingine ya nyanya pia tuna mkate wa lishe ambayo umetengenezwa kwa Ngano ambayo haijakobolewa, maharage ya soya hii yote ni kuhakikisha mtumiaji anapata virutubisho ambavyo ni vizuri vilevile tunamwambia mwananchi tunatoa Elimu ya muda mfupi na kwa bei nafuu, hivyo wiki moja, tatu au mwezi mmoja anapata elimu yake na kujikwamua kiuchumi”.amesisitiza Bw. Masinga.

Post a Comment

0 Comments