NA:Winfrida Nicolaus
Wananchi wa Morogoro na Kanda
ya Mashariki wametakiwa kutembelea banda la SUA kwenye Maonesho ya 29 ya
Wakulima, Wafugaji na Wavuvi ili kujifunza na kujionea baadhi ya Bidhaa ambazo
zimefanyiwa Utafiti kutoka kwenye Miti na kutengeneza dawa ambazo zinatibu
Magonjwa ya aina mbalimbali.
Amesema hayo Mtaalam wa Maabara
kutoka Idara ya Fiziolojia, Biokemia na Famakolojia, Ndaki ya Tiba ya Wanyama
na Sayansi ya Afya katika Chuo cha Sokoine cha Kilimo SUA Bw. Ignatus Kiiza
wakati akizungumza moja kwa moja na SUA Radio kutoka kwenye Viwanja vya
Maonesho hayo.
Amesema kuna aina mbalimbali za
dawa ambazo zimetoka kwenye miti ambayo imefanyiwa utafiti na kuweza kutibu
magonjwa endapo mtu akitumia kwa usahihi anaweza kupona kabisa ambapo dawa hizo
ni pamoja na Wound Spray ambayo kazi yake kubwa ni kutibu Vidonda vipya,
vidonda vilivyotokana na magonjwa kama ya Kisukari, vilivyotokana na Moto na
vile ambavyo vimekaa muda mrefu.
Bw. Kiiza amesema aina nyingine
ya dawa inaitwa Wound Gell ambayo ipo kwenye mfano wa mafuta na kazi yake kubwa
ni kutibu Magonjwa ya Ngozi yaani Fungus, Mapunye au Mashiringi pamoja na
harara hivyo mtu mwenye matatizo kama hayo akipata dawa hizo zitamsaidia kwa
muda mfupi na kumuwezesha kupona kabisa.
Vilevile kuna sabuni ambayo
inatumika kama dawa kwa njia ya kuogea ambapo
mtu anaweza kuitumia kwa kutibu Magojwa ya Ngozi na kuilinda Ngozi yake .
“Kuna Product yaani bidhaa za dawa ambazo zimetokana na miti ambayo
imefanyiwa utafiti na dawa hizo zinaweza kutibu magonjwa ya aina mbalimbali
kama vile vidonda vya muda mrefu au vipya, vidonda vya moto na vile kama mtu wa
kisukari akipata hivyo kuna dawa iitwayo Wound Gelly ambayo mtu akiitumia
anapona kwa muda mfupi”, ameeleza zaidi Bw. Kiiza.
Aidha Bw. Kiiza amewataka
watanzania kutembelea banda la SUA kwenye Maonesho hayo ya 29 ya Wakulima,
Wafugaji na Wavuvi kujipatia bidhaa hizo lakini pia kutembelea chuo cha SUA
kutoka Idara ya Fiziolojia, Biokemia na Famakolojia ili wajipatie dawa hizo na
kupatiwa elimu kuhusiana na namna bora ya kuzitumia pamoja na faida zake.




0 Comments