SUAMEDIA

SUA yatoa Elimu kuhusu Teknolojia rahisi, Rafiki kwa kudhibiti Panya

 

NA: Winfrida Nicolaus

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kupitia Taasisi ya Kuthibiti Viumbe Hai Waharibifu inatoa Elimu kuhusiana na Teknolojia rahisi na Rafiki kwaajili ya kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu hasa Panya katika Maonesho ya 29 ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi Kanda ya Mashariki.


Amesema hayo Mtafiti Msaidizi kutoka Taasisi hiyo Dkt. Amina Ramadhani Issae wakati akizungumza Mubashara kupitia SUA Radio kutoka katika Viwanja vya Maonesho ya 29 ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi Kanda ya Mashariki.

Amesema katika maonesho hayo wanaonesha Teknolojia mbalimbali za kudhipiti Viumbe Hai Waharibifu kama Panya ikiwemo Teknolojia ya kutumia Bundi katika kudhibiti Panya Shambani, Mitego ya aina mbalimbali ya kutegea panya ambayo inatengenezwa na Taasisi hiyo lakini pia Teknolojia ya Kudhibiti Panya Majumbani ikiwemo Mbinu ya kutumia Mkojo wa Paka kwaajili ya kufukuza Panya ndani ya nyumba.

Dkt. Amina amesema licha ya wananchi kuona Teknolojia mbalimbali za kudhibiti Panya vilevile wanaelimishwa kuhusiana na Madhara ya Panya katika kusambaza Magonjwa kwa binadamu na hata Wanyama wengine lakini pia Panya haohao licha ya kusababisha madhara wamekuwa na faida kama vile kuokoa Maisha ya Binadamu ikiwemo kugundua Vimelea vya Magonjwa kama TB, Kugundua Mabomu yaliyotegwa Ardhini Pamoja na kutambua harufu za binadamu waliofukiwa na vifusi.

Amesema Bundi ana uwezo wa kula Panya mmoja hadi kumi na mbili kwa siku hivyo katika kudhibiti Panya kwa kutumia Bundi anachotakiwa kufanya Mkulima ni kutengeneza mazingira Rafiki yanayomuwezesha bundi kutua katika shamba lake ikiwemo kutengeneza viota vya mbao vyenye tobo na kuvining”iniza kwenye nguzo ambapo vitamuwezesha bundi huyo kutua na kukabiliana na panya katika shamba lake.

Katika banda la SUA Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu kuna mambo mbalimbali hasa Teknolojia ya Kuthibiti Panya Mashambani vilevile kuwaeleza wananchi au watu wanaotembelea banda letu Madhara ya Panya lakini kama chanzo cha kusambaza Magonjwa kwa binadamu na hata wanyama wengine lakini wamekua na faida nyingi licha ya kusababisha majanga kuna wanaosave Maisha ya binadamu mfano Panya wanaogundua Vimelea vya Magonjwa kama TB ”, amesema Dkt. Amina .

“Pia kuna Panya ambao wanaweza kugundua Mabomu yaliyotegwa Ardhini na ambao wamefundishwa kuokoa watu ambao wamepata Majanga kama vile kuangukiwa na vifusi au magorofa sasa kuna wale Panya ambao wamefundishwa jinsi ya kutambua harufu ya binadamu ambao wamenasa ndani ya vifusi”, ameongeza Dkt. Huyo.

Aidha lengo la kuja kwenye Maonesho hayo ya 29 ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi ni kuwaelimisha wananchi hivyo amewasisitiza kutembelea Banda la SUA hasa katika Taasisi ya Kuthibiti Viumbe Hai Waaribifu kujifunza ili waweze kudhibiti viumbe hao bila ya kutumia kemikali.








Post a Comment

0 Comments