SUAMEDIA

Taasisi ya Kuwajengea Uwezo Wajasiriamali, tayari kuwafikia Wajasiriamali na Wakulima katika harakati zao za kujiletea maendeleo

 

NA:Winfrida Nicolaus

Taasisi ya Kuwajengea Uwezo Wajasiriamali katika harakati zao za kujiletea Maendeleo (AICAD) imeendelea na kazi yake ya kuwajengea uwezo Wajasiriamali pamoja na Wakulima kwa kutumia Teknolojia zinazozalishwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA ili kuwawezesha wakulima hao kujikwamua na hali duni ya kimaisha.



Amebainisha hayo Afisa Programu wa AICAD Bw. Florence Rugimbana Agosti 06, 2022 wakati akizungumza mubashara kupitia SUA Radio kutoka kwenye viwanja vya Maonesho ya 29 ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi Kanda ya Mashariki yanayofanyika Mkoani Morogoro.

Amesema Taasisi ya Kuwajengea Uwezo Wajasiriamali (AICAD) inafanya kazi zake kwa kushirikiana na Vyuo Vikuu Pamoja na Taasisi zingine zinazozalisha Teknolojia mbalimbali ambapo kazi yake haswa ni kuweka daraja kati ya wazalishaji Teknolojia ambao ni vyuo vikuu ikiwemo SUA.

Bw. Rugimbana amesema lengo la kufanya mashirikiano na SUA ni kutumia Teknolojia ambazo wanazizalisha hasa katika Kilimo kuwajengea uwezo wajasiriamali kwa kuwapatia mafuzo na wao kuyatumia ili kujikwamua kiuchumi.

Aidha amesema Taasisi ya AICAD pia inafanya Tafiti mbalimbali kwenye jamii kuona wanakabiliana na changamoto gani au wanarasilimali zipi ambapo baada ya kuzitambua wanarudi kwenye taasisi ambazo zinazalisha Teknolojia ili kupata majibu ya namna ya kutatua changamoto hizo ikiwemo kwa Wakulima, Wafugaji pamoja na Wajasiliamali kwa ujumla.

“Tumekuja kwenye Maonesho haya ya 29 hapa kwenye banda la SUA ili kuwaeleza wananchi AICAD ni nini, kuonesha baadhi ya bidhaa kutoka kwa wajasiriamali ambao wamefuzu kozi zetu mbalimbali ambazo tunazitoa ikiwemo Usindikaji na Uongezaji wa thamani wa Mazao ya Kilimo, Uongezaji na Uboreshaji wa Kazi za Mikono vyote hivyo vimetolewa na AICAD”, amesema Bw. Rugimbana.

 Amesema kuwa mwanazoni walianza kwa kuelimisha vikundi mbalimbali lakini sasa wataanza kutoa mafunzo kwa mtu mmoja mmoja kutokana na uhitaji wa watu.

Ameongeza kuwa AICAD inatoa Mafunzo mbalimbali ya siku 10 hadi 15 pia wana machapisho kutoka kwenye tafiti mbalimbali ambazo wamezifanya pamoja na vitini kwaajili ya Mafunzo zaidi.

 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments