SUAMEDIA

Watumishi wa Umma waaswa kuwa Kioo katika kuzingatia Maadili

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewaasa watumishi wa umma kuwa na maadili ili kujenga taswira nzuri ya Serikali kwa wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa huduma zitolewazo na taasisi za umma nchini. 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi katika halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao wa umma.

Mhe. Ndejembi ametoa wito huo kwa watumishi wa umma nchini, wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, akiwa katika ziara ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamozo zinazowakabili watumishi wa umma katika Wilaya hiyo ya Monduli.

Mhe. Ndejembi amesema watumishi wa umma ndio kioo cha jamii, na ni taswira ya Serikali katika jamii, hivyo wanapaswa kuwa na maadili mema yatakayolinda haiba ya Serikali na utumishi wa umma kwa ujumla.

Aidha, Mhe. Ndejembi amewataka watumishi wa umma kuzingatia utunzaji wa siri za Serikali wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku, ili taarifa na nyaraka za Serikali ziendelee kuwa katika mikono salama ya Serikali yenyewe.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. Frank Mwaisumbe amemshukuru Mhe. Ndejembi kwa kuhimiza uadilifu kwa watumishi wa wilaya yake, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu na ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kiutumishi.

Naye, Afisa Maendeleo ya Jamii, Bi. Rose Mhina kwa niaba ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, amemshukuru Mhe. Ndejembi kwa kusikiliza kero na changamoto zinawakabili na kuzifanyia kazi papo kwa hapo, ikiwa ni pamoja na kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali za kiutumishi walizoziwasilisha. 



Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. Frank Mwaisumbe akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya yake, wakati wa ziara  ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.



Afisa Elimu Taaluma Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Bi. Restiel Mselli (aliyesimama) akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa halmashauri hiyo.

Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Bw. Emmanuel Kipimo (aliyesimama) akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa halmashauri hiyo ya Monduli.

Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Bi. Rose Mhina akitoa neno la shukurani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi, wakati wa ziara yake ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Monduli.

Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao wa umma.

James K. Mwanamyoto

Afisa Habari-UTUMISHI

0713 360 813

14/07/2022.

Post a Comment

0 Comments