SUAMEDIA

Urusi kupeleka mfumo unaofyatua makombora ya nyuklia Belarus

 


Rais wa Urusi Vladimir Putin ameahidi kupeleka mifumo ya Iskander-M inayoweza kufyatua makombora ya nyuklia nchini Belarus. Haya yamejiri mnamo wakati vikosi vya Urusi vimechukua udhibiti kamili wa mji wa Sieverodonetsk.

Urusi inanuia kupeleka mifumo kwa jina Iskander-M inayoweza kufyatua makombora ya nyuklia nchini Belarus katika miezi michache ijayo. Rais Vladimir Putin alisema hayo Jumamosi kupitia televisheni ya Urusi wakati wa kuanza kwa mkutano kati yake na kiongozi wa Belarus Alexander Lukashenko mjini Saint Petersburg.

Putin alisema pia Urusi itaisaidia Belarus kuboresha ndege zake za kivita aina ya Su-25 kuziwezesha kubeba silaha za nyuklia.

Rais wa Belarus Lukashenko alielezea wasiwasi wake kuhusu kile alichokiita uchokozi na será za kuudhi za majirani zake Lithuania na Poland.

Alimuomba Putin kuisaidia Belarus kuwa na ‘majibu yanayofanana' na kile alichosema kuwa ndege za kivita za nyuklia zinazoongozwa na Jumuiya ya Kujihami ya NATO, karibu na mpaka wa Belarus

Post a Comment

0 Comments