SUAMEDIA

UNICEF: Utapiamlo wawaweka watoto milioni 8 katika hatari ya kifo

 



Shirika la Umoja wa Mataifa linalishughulikia watoto, UNICEF limesema leo kwamba karibu watoto milioni 8 wa umri wa miaka mitano na chini ya hapo wako hatarini kufa kutokana na utapiamlo wa utotoni. 

Kulingana na UNICEF watoto walioathirika zaidi wanatokea kwene mataifa 15 ambayo kwa sasa yana upungufu mkubwa wa chakula. Mataifa hayo ni pamoja na Afghanistan, Ethipoa, Haiti na Yemen, ambayo yote yanahitaji msaada wa dharura wa chakula na vifaa tiba. 

Limeongeza kuwa watoto wengi wanaingia kwenye kitisho hicho kwa kuwa utapiamlo unaongezeja kia dakika. 

Matatizo yanayochangia ni pamoja na kuongezeka kwa bei za vyakula uliochochea zaidi na vita vya Ukraine, ukame katika baadhi ya mataifa na athari endelevu za janga la UVIKO-19. 

Shirika hilo limesema kunahitajika dola bilioni 12 ili kuzuia athari zaidi.

Post a Comment

0 Comments