Tafiti zinaonyesha raia 1 kati ya 5 wa Marekani aliyewahi kuambukizwa UVIKO-19 bado anaonyesha dalili za muda mrefu za maambukizi.
Tawimu zilizokusanywa katika kipindi cha wiki mbili za kwanza za Juni zinasema idadi hiyo ni ya watu wazima.
Maafisa wa afya wa Marekani wanasema mtu mzima 1 kati ya 13 nchini humo huwa na dalili zinazodumu kwa miezi mitatu ama zaidi baada ya kupata maambukizi kwa mara ya kwanza, na ambazo hakuwahi kuonyesha kabla ya kuambukizwa.
Dalili hizo ni pamoja na uchovu wa muda mrefu, mapigo ya moyo kwenda kasi, kukosa pumzi, matatizo kwenye njia ya hewa, maumivu yaasiyotibika ya kifua na udhaifu wa misuli.
Takwimu hizo zilikusanywa na ofisi ya takwimu kati ya Juni 1 na 13 na kuchambuliwa na Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa, CDC na wahanga wakubwa wakiwa ni raia kutoka Uhispania.
0 Comments