Vedasto George
SUA
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Sokoine Cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda amewataka wafanyakazi kufanya
kazi kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za kiutumishi ili chuo hicho kiweze
kufikia malengo yaliyowekwa.
Prof. Chibunda akihutubia wafanyakazi wa SUA siku ya Mei Mosi
Prof. Chibunda ametoa wito huo
wakati akitoa hotuba yake kwenye siku ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi
kwenye ukumbi wa chuo wa Multipurpose ambapo amesema kuwa njia pekee ambayo inaweza
kupelekea chuo kufikia malengo yake ni wafanyakazi kuakikisha wanafanya
kazi kwa bidii pasipo kuwa na uzembe wa aina
yeyote.
“Nitoe wito kwa wafanyakazi wote, tufanye
kazi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu na uadilifu mkubwa, hili suala la uadilifu muda mwingine
lina changamoto zake ninafahamu bado
hapa chuoni kuna vitengo vyetu ambavyo vinatuumiza zaidi sisi wenyewe lakini vingine vinakiumiza chuo chetu na hasa wadau wetu wa nje, kuna malalamiko makubwa mfano kwa wenzetu
kitengo cha Ununuzi kuna ucheleweshaji,
ununuzi wa vitu ambavyo bei yake inaitia hasara serikali kupitia chuo lakini bado kuna malalamiko ya matumizi ya
lugha chafu kwa watu. Amesema Prof.Chibunda.
Mmoja wa wafanyakazi bora akipokea cheti kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Chama cha Wafanyakazi RAAWU tawi la SUA Faraja Kamendu amesema siku ya wafanya
kazi duniani ni siku ambayo inatumiwa
kwa ajili ya ukumbusho wa mafanikio ya
kijamii na kiuchumi ikiwa ni matokeo chanya yaliyoletwa na vuguvugu la
wafanyakazi lililotokea karne ya 18.
Kamendu ameuomba uongozi na
menejimenti ya chuo kuharakisha mchakato wa kuwapatia mafao baadhi ya watumishi
waliopoteza sifa ya utumishi na
kuondolewa kazi baada kukosa sifa ya elimu ya kidato cha nne hasa wale ambao waliajiriwa baada ya waraka wa serikali wa mei 4 mwaka
20004.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi RAAWU tawi la SUA Faraja Kamendu akizungumza katika sherehe ya wafanyakazi SUA
“Watu hawa tunajua
waliitetea SUA na waliisaidia kwa sehemu
kubwa na watu hawa waliandika barua
angalau kuomba kama kuna kitu chochote
wanaweza wakapata hasa kwenye mifuko yao
ya kijamii” Amesema Kahedu
Naye Kaimu Katibu wa Chama cha
Wafanyakazi RAAWU tawi la SUA Farida Mkongwe Kurunge wakati akisoma risala ya
wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA mbele ya Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho amesema ili
wafanyakazi waweze kuwa na mshikamano imara ni lazima kuwepo na
ushirikiano baina ya wafanyakazi na
mwajiri ikiwemo pia ushirikishwaji katika kutoa maamuzi kwenye masuala mbalimbali ya chuo.
Kaimu Katibu wa Chama cha Wafanyakazi RAAWU tawi la SUA Farida Mkongwe Kurunge akisoma risala ya wafanyakazi mbele ya Mgeni Rasmi
“Unaposhirikishwa katika
kutoa maamuzi inapelekea utekelezaji wa
majukumu kuwa mwepesi kwani unakuwa unatekeleza maamuzi yako, wafanyakazi
wanapotimiza wajibu wao ipasavyo
wanakuwa na matumaini ya kupata
stahiki zao kwa wakati hivyo tunashauri na kuhimiza
kila mfanyakazi atimize wajibu wake kwa mwajiri” Amesema Farida
Mkongwe
0 Comments