Serikali ya Tanzania imesema imeanza mchakato wa kuunganisha
kitambulisho cha Taifa na kitambulisho cha mpiga kura ili kumfanya mtanzania
kutumia kitambulisho cha taifa katika zoezi la kupiga kura
Akiuliza swali bungeni leo mbunge wa Kawe Askofu Josephati
Gwajima alitaka kujua kama Serikali haioni umuhimu wa kuunganisha mifumo ya
Kitambulisho cha Mpiga Kura na Kitambulisho cha Taifa ili kuepusha usumbufu kwa
Wananchi,
Akijibu swali hilo kwa niaba ya waziri wa mambo ya ndani Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamis Hamis amesema
serikali imeanza mchakato wa kuunganisha vitambulisho hivyo viwili na kufanya
sasa mtanzania kutumia kitambulisho cha taifa katika mchakato wa Uchaguzi wa
kawaida na ule wa kieletroniki ‘e-voting’.
Naibu waziri Hamis amesema kuwa Matumizi hayo yatapunguza
gharama kwa Serikali katika kuandikisha na kutengeneza daftari pamoja na
kurahisisha usimamizi wa wapiga kura.
Ameeleza kuwa Mawasiliano kati ya Taasisi hizo mbili yenye
dhumuni la kuiwezesha kanzidata ya NIDA kutumika katika zoezi la uboreshaji wa
Daftari la Wapiga Kura yameanza mwezi Machi, 2022.
CHANZO MUUNGWANA
0 Comments