TAASISI ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) ya Dar es Salaam imefanya
upasuaji wa ubongo bila kufungua fuvu kwa zaidi ya wagonjwa 120 katika mwaka
mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa
Muhimbili (MOI), Dk Respicious Boniface alisema hayo jijini Dar es Salaam
wakati akieleza mafanikio ya taasisi hiyo katika mwaka mmoja wa Serikali ya
Awamu ya Sita.
Alisema kuwa kabla ya mashine ya kupasua bila
kufungua fuvu (Angio Suite), wagonjwa walikuwa wanapelekwa nje ya nchi huku
gharama za matibabu zikiwa ni Sh milioni 30 hadi 60 lakini hapa nchini huduma
hiyo ni Sh milioni 10 hadi 15.
Dk Boniface alisema kuwa kupitia huduma hiyo
wagonjwa wamekuwa hawakai muda mrefu hospitalini hivyo gharama zinapungua.
Mashine hiyo iligharimu Sh bilioni 7.9 na huduma ilianza kutolewa Januari 26,
2021.
“Zamani kabla ya kuanza kufanya upasuaji huu
ulikuwa unafungua ili ufike inachukua saa sita kwenye ubongo sasa unatumia saa
moja hadi moja na nusu,” alisema na kuongeza kuwa mgonjwa anakuwa hana kidonda
kikubwa hivyo anakaa muda mfupi.
Gharama yake nje ya nchi ni Sh milioni 40 lakini
ndani ya nchi ni Sh milioni nane.
Alisema mafanikio mengine ni ununuzi wa mashine
sita za kusaidia kupumua na vitanda 12 vya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)
kupitia fedha za mgawo wa Covid-19.
Ufungaji wa mashine kwa ajili ya kupasua bila
kufungua fuvu (Angio Suite) uligharimu kiasi cha Sh bilioni 7.9 ambapo huduma
hiyo ilianza kutolewa Januari 26, 2021.
CHANZO MUUNGWANA
0 Comments