Na Gerald Lwomile
Morogoro
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia
Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE) kimefanikiwa kuwafundisha zaidi ya vijana 300 kutoka Kata tisa ikiwemo Kilakala na Boma mafunzo ya uoteshaji na uzalishaji wa miti ya matunda kibiashara,
ufugaji wa kuku, ufugaji wa samaki na ujasiriamali
Hayo yamesemwa mkoani Morogoro na Mkuu wa Kitengo cha
Ugani ICE-SUA Dkt. Innocent Babili wakati akizungumza na SUA Media mapema wiki
hii ili kujua ni kwa namna gani wazalishaji wa miche ya matunda wamenufaika na
mafunzo hayo
Dkt. Babili amesema katika mafunzo ambayo wameyatoa
hivi karibuni vijana mbalimbali kutoka kata ya Kilakala na Boma wamejifunza
namna bora ya kuotesha na kuzalisha miche ya matunda kibiashara
“Mafunzo haya ni moja ya majukumu ambayo ICE imefanya
kwa mwaka 2021/2022 lakini pia tumekuwa tukitoa mafunzo ya aina mbalimbali kama
ufugaji wa kuku na ufugaji wa Samaki na hata watafiti na hii inadhihirisha kuwa
SUA ni hazina ya kilimo” amesema Dkt. Babili
Wakizungumzia mafunzo hayo vijana Evarist Luvanda na
Suzan Fabian wakazi wa mtaa wa Mahedu kata ya Kilakala Manispaa ya Morogoro
wamesema mafunzo hayo yamewasaidia katika kufuhamu mambo mbalimbali kama
ujasirimali, uoteshaji na uzalishaji wa miche ya matunda
“Mimi nimejifunza mambo mengi sana ambayo awali
sikuyajua nimejifunza namna ya uoteshaji wa miche na ubebeshaji kitaalamu
wanaita ‘budding’ na unaweza kubesha mfano mlimao kwa mchungwa” amesema
Suzan
Mafunzo hayo yametolewa na SUA kwa kushirikiana na
SWISSCONTACT na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, mbali na vijana hao kupata
mafunzo lakini pia wamepata vyeti ambayo vimethibitisha ushiriki wao
0 Comments