Na
Flora Rugaimukamu
DSJ
Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kimesema kitaendelea kutoa elimu ambayo itawasaidia wafugaji wa samaki kujua namna ya kuwatunza na namna ya kuwapa virutubisho ambavyo vitasaidia ukuaji wa viumbe hao.
Akizungumza na SUAFM 101.1 leo Machi 09, 2022 Mhadhiri Msadizi
kutoka Kitengo cha Ukuzaji wa Viumbe SUA Bi. Mariam Bakari amesema ili kusaidia
ukuaji bora wa samaki mfugaji anatakiwa kuhakikisha samaki wanapata matunzo
bora hasa usafi wa maji ambayo ndiyo makazi ya viumbe hao na kupata vyakula
vyenye virutubisho ambavyo vitasaidia
katika ukuaji wao.
Amesema vyakula vyenye virutubisho kwa samaki husaidia
katika ukuaji bora wa viumbe hai, na kuongeza kuwa virutubisho hivyo vinakuwa
na protini, wanga, vitamini na madini
pia ameshauri samaki kupata mwanga wa jua ambao husaidia kuzalisha chakula cha
asili.
"Samaki ili kuweza kukua wanahitaji vyakula
vyenye virutubisho vyote ambavyo vimegawanyika katika makundi mbalimbali, chakula
kimojawapo ni chakula asili ambacho hiki upatikana ndani ya maji" amesema
Bi Mariam Bakari
Hata hivyo mtaalamu huyo amewataka wafugaji kuwa
makini katika ulishaji wa samaki na pia umakini katika usafi maji na kuwa ni
muhimu kubadili maji pindi yanapokuwa machafu ili kuzuia vifo vya samaki.
"Ningependa kutoa ushauri wafugaji wa samaki kuwa
makini hasa katika upande wa chakula ili kuwezesha samaki kukua wanatakiwa
kupata vyakula vyenye virutubisho vyote na ili kuepusha vifo vya samaki ni
muhimu kuhakikisha samaki wanaishi katika maji masafi na kipindi cha mvua
tunashauri mfugaji kutengeneza uzio ambao utazuia maji machafu kufika katika
makazi ya viumbe hao” amesema Bi. Mariam
0 Comments