Diana Bundala maarufu kama ‘Mfalme Zumaridi' na wenzake 92 leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Mwanza wakikabiliwa na kesi tatu ikiwamo ya usafirishaji haramu wa binadamu.
Makosa mengine ni pamoja na shambulio la kudhuru mwili na
kuzuia maofisa wa Serikali kutimiza wajibu wao.
Akiwasomea mashitaka hayo mahakamani hap oleo Machi 3,
Mwendesha mashtaka wa Serikali amesema katika kesi namba 10/2022 inayomkabili
Mfalme Zumaridi peke yake, akidaiwa kusafirisha binadamu wakiwemo watoto wenye
umri chini ya miaka 18 kinyume cha kifungu namba 4(1) (A) na 6(2) (A) cha
sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu namba 6 ya mwaka 2008.
Katika kesi namba 11/2022, Luvinga amesema Mfalme Zumaridi na
wenzake wanane wanadaiwa kufanya shambulio la kudhuru mwili askari wa Jeshi la
Polisi waliofika nyumbani kwake kutekeleza wajibu wao kinyume cha kifungu namba
241 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.
Washtakiwa hao pia wanadaiwa kuwazuia maofisa wa Serikali
kutimiza wajibu wao kinyume cha kifungu namba 114(A) kifungu kidogo B cha
Kanuni ya Adhabu.
Katika kesi namba 12/2022, mwendesha mashataka huyo ameiambia
Mahakama mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, Monica
Ndyekubora kuwa Zumaridi na wenzake 92 wanadaiwa kufanya kusanyiko lisilo
halali kinyume cha kifungu cha 74(1) na 75 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.
Kuhusu shauri namba 10 la usafirishaji haramu wa binadamu
linalomkabili Mfalme Zumaridi, mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kutokana na
Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria kusikiliza kesi hiyo.
Licha ya mashtaka namba 11 na 12 kuwa na dhamana huku baadhi
ya ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wamejitokeza kuwadhamini, washtaki wote
wanaowakilishwa na Wakili Erick Mutta walikataa dhamana wakisisitiza kuwa wako
tayari kwenda mahabusu kuungana na kiongozi wao anayekabiliwa na kesi ya
usafirishaji haramu wa binadamu isiyo na dhamana.
Kutokana na uamuzi huo, Hakimu Ndyekubora ameamuru washtakiwa
wote kupelekwa mahabusu hadi Machi 17, shauri hilo litakapotakwa kwa ajili ya
washatakiwa kusomewa maelezo ya awali katika shauri namba 11 na 12.
0 Comments