SUAMEDIA

Waziri Masauni ayataja mambo mawili yanayomkosesha usingizi, mauaji, Polisi wanaojihusisha na uhalifu nchini

 Na WMNN, Kilimanjaro.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema matukio ya mauaji yanayoendelea nchini pamoja na Polisi wanaojihusisha na matukio ya uhalifu yanamfanya hakose usingizi hivyo amewataka askari kuwa waadilifu.


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akizungumza na askari wanaotarajia kuhitimu kozi ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisibnkatika kambi ya kivita ya kambapori iliyopo wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 


Ameongeza kuwa tangu ateuliwe kuiongoza Wizara hiyo ambapo sasa amefikisha mwezi mmoja lakini masuala ya mauaji pamoja na baadhi ya polisi kushiriki katika masuala ya uhalifu yanamkosesha usingizi na pia hata Rais Samia Suluhu Hassan naye anakosa suingizi kutokana na matukio.

Waziri Masauni amzungumza hayo katika Kambi ya Kambapori, Wilayani Siha, Mkoa wa Kilimanjaro, leo, wakati alipokuwa anaangalia maonesho ya kivita yaliyokuwa yanafanywa na wanafunzi wa mafunzo ya wakaguzi wasaidizi wa polisi, ambapo anatarajia kufunga mafunzo hayo Februari 11, 2022, Wilayani Hai, Mkoani humo.

“Mimi tangu nimeingia kipindi hiki cha muda mfupi kama mwezi mmoja hivi, kuna vitu wiwili vikubwa vinanikosesha sana usingizi, na si mimi tu nina uhakika Amiri Jeshi Mkuu Rais Samia Suluhu Hassan, nina uhaki anakosaa usingizi, na pia na Watanzania wote walioweme, wazalendo wanaoipenda nchi yao, watakua wanakosa usingizi, matukio yenyewe la kwanza ni mauaji, mara utasikia kachinjwa mtu, ukiuliza sababu unaambiwa sababu ya mapenzi, mara kaenda kwa mganga kadhulumiwa,” alisema Masauni.

Ameongeza kuwa watu wananchukua sheria mkononi, jambo hilo halikubaliki, hivyo wanafunzi hao wanaohitimu mafunzo hayo ya wakaguzi wasaidizi wanatarajiwa kwenda katika Kata watakazopangiwa ili waweze kuyamaliza matukio hayo kwasababu hayakubaliki katika jamii.

“Na nyinyi ambao mnatarajiwa muhitimu, nimeambiwa na IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi) hapa, nyie mnaenda kupewa nafasi ya uongozi katika ngazi ya kata na kadhalika, mna nafasi kubwa sana ya kwenda kutusaidia, kuisaidia nchi yenu, kazi hii sio ya kwenu peke yenu, kwasababu leo ametoka huko na wivu wakle ndani yar oho, mnachotakiwa nyie kufanya utaratibu kumkamata, sisi tunataka kudhibiti matukio kama haya yasiendelee ili kazi yenu iwe nyepesi, lazima mnapokwenda kule mtumie elimu yenu mlioipata leo, sio tu elimu ya kijeshi lakini elimu ambayo hata mnayoipata katika mafunzo ya nadharia ambayo najua itakua mambo mengi ikiwemo kujopanga vizuri kwa kushirikiana na wenzenu kutumia kila taaluma ya taasisi ili kudhibiti matukio ya mauaji yasiendelee katika nchi hii, kwakuwa hili jambo linasonesha Taifa na lazima likome” alisema Masauni.

Aidha, Masauni alisema jambo la pili kwa muda wake wa mwezi mmoja linalomkosesha usingizi ni vitendo vya baadhi ya askari Polisi kufanya vitendo kinyume na maadili jambo ambalo halikubaliki katika Jeshi hilo.

“Kumekuwepo na baadhi ya polisi wachache ambao wanaotia doa Jeshi hili, lakini ambao wanafanya kazi yenu kuwa ngumu, kwasababu kunapotokea na mtu ambaye ni askari anafanya mambo ya hovyo kinyume na maadili alafu mwananchi anakimbilia wapi sasa, anaweza kusema askari wote wapo hivi kumbe askari wengi wapo ni wazuri tu, wazalendo na wasafi, na wanafnaya kazi usiku na mchana hawalali kwa ajili ya nchi hii,” alisema Masauni na kuongeza;

“UItakuta askari anashiriki kuiba fedha za mwananchi, askari leo anatoa siri, utakuta katika kituo cha polisi anampigia simu mhalifu, kaja leo fulani kukuchoma, askari leo wapo wala rushwa wakubwa, lazima sisi viongozi tuwaambie, matukio haya yanaweza kufanya nchi hii isiwe salama, nyie mnakwenda huko katika maeneo yenu, mtumie taaluma yenu mlioip[ata hapa, mimi nina uhakika taaluma inayotolewa hapa ni nzuri, nap engine hao wanaofanya hay ani kwa bahati mbaya wamepenye humu kaingia kumbe huko alikua mwizi, mkafichue hao ili wachukuliwe hatua za kisheria na ambao haya yakome ndani ya jeshi la polisi.”

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro amesema kuwa, Jeshi la Polisi limejipanga kukabiliana na matishio mbalimbali ikiwemo wa kutumia silaha za moto na kwamba hakuna mhalifu atakayefanikiwa kutekeleza tukio la kihalifu.

Pia Waziri aliwaambia askari hao kuwa wapo katika mafunzo hayo kutokana na Rais Samia kuwapenda na kufanikisha kupata mafunzo hayo muhimu katikia Jeshi, hivyo waendelee kufanya kazi za kizalendo, na pia alimpongeza Mkuu wa Jeshi hilo pamoja na wasaidizi wake kwa kuandaa mafunzo hayo.



WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akizungumza na askari wanaotarajia kuhitimu kozi ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi katika kambi ya kivita ya kambapori iliyopo wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, leo. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 



WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (kulia), akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro, wakati alipokuwa anawasili katika kambi ya kivita ya Kambapori iliyopo wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 




Post a Comment

0 Comments