Na: Gerald Lwomile
Katavi
Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini wakiwemo wale wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wametakiwa kuzingatia maadili na hasa katika mavazi ili kulinda utamadumi wa Mtanzania
Prof. Yasinta Muzanila akishiriki katika kiapo cha uadilifu |
Akizungumza na wanafunzi wa
SUA Kampasi ya Mizengo Pinda mkoani Katavi, Katibu wa Kamati ya Kuthibiti
Uadilifu SUA (KKU) Prof. Yasinta Muzanila amesema pamoja na kuwa vijana wengi
wanapenda kuwa kisasa lakini wanaweza kuwa katika hali hiyo huku wakilinda
utamadani wa Mtanzania
“Ni kweli unaweza kuvaa
suruali yako nzuri ya dangrisi au kadeti na ukaivaa vizuri tu bila kuishusha
kwenye sehemu ya makalio, lakini pia kwa kina dada unaweza kuvaa blauzi yako
nzuri ya kisasa kabisa pasipo kuacha kifua chako wazi” amesema Prof. Muzanila
Naye mjumbe wa kamati hiyo
Bi. Lightness Mabula amewataka wanafunzi kuhakikisha wanajiepusha na ngono
wawapo chuoni kwani jambo hilo linaweza kuwasababisha wakashindwa kufikia
malengo yao
Amesema mbali na kushindwa
kufikia malengo lakini pia wanaweza kupata magonjwa ya zinaa kama Ukimwi,
Kaswenda, Ngono na hata kupata mimba au Watoto katika kipindi kisichotarajiwa
Awali Mwenyekiti wa KKU SUA
Prof. Christopher Mahonge amewakumbusha wanafunzi kujua namna bora ya kupanga
muda wao ili kuhakikisha wanafanya kile kilichowapelekea chuoni
Amesema watu wengi wameshindwa
kufanya na kutimiza malengo yao kutokana na kushindwa kupanga muda wao na
kupelekea kushindwa kutimiza malengo yao.
0 Comments