SUAMEDIA

Wanasayansi wa Australia washangazwa na kitu cha kutisha kinachozunguka anga za mbali

 

Wanasayansi wa Australia washangazwa na kitu cha kutisha kinachozunguka anga za mbali

CHANZO CHA PICHA,ICRAR / CURTIN

Maelezo ya picha,

Wanasayansi wa Australia washangazwa na kitu cha kutisha kinachozunguka anga za mbali

Wanasayansi wa Australia wanasema wameona chombo kisichojulikana kinachozunguka eneo la anga za mbali ambacho ni tofauti na vitu vingine katika anga hiyo.

Chombo hicho kilichogunduliwa na mwanafunzi wa chuo kikuu, kinatajwa kutoa viwango vya juu vya mawimbi ya miale kila baada ya dakika 18

Vitu vinavyotoa nishati katika anga za mbali vimegunduliwa kwa kiasi kikubwa. Lakini watafiti wanasema kitu ambacho hutetemeka kwa dakika moja sio jambo la kawaida sana.

Uchunguzi zaidi unaendelea

Chombo hicho kiligunduliwa kwa mara ya kwanza na mwanafunzi anayefanya kazi katika mradi wa darubini ya redio inayoitwa 'Murchison Widefield Array' katika eneo la jangwa lisilo na watu la Australia Magharibi.

Tyrone O'Dwyer, mwanafunzi aliyehitimu kutoka Chuo Kikuu cha Curtin, aligundua chombo hicho kupitia darubini na mbinu mpya aliyobuni.

O'Doharty ni mwanachama wa timu inayoongozwa na Dk. Natasha Hurley-Walker, mtaalamu wa anga katika kituo cha kimataifa cha utafiti wa Astronomia (ICRAR) katika Chuo Kikuu cha Curtin.

"Wakati wa uchunguzi wetu, kilionekana na kutoweka kwa saa kadhaa," alisema katika taarifa ya ICRAR iliyotolewa kwa vyombo vya habari.

"Haitarajiwi kabisa na inatisha kwa mwanaastronomia yeyote,kwa sababu hatukuwahi kujua chochote kuhusu chombo cha angani kuwa na tabia kama hii."

ICRAR iliongeza kuwa baada ya majaribio ya data, timu iliweza kuthibitisha kuwa chombo hicho kilikuwa takriban miaka 4,000 kutoka kwa dunia na kilikuwa na sumaku yenye nguvu sana.

Kufikia sasa, nadharia zimependekeza kuwa chombo hicho kinaweza kuwa nyota ya nyutroni au mabaki ya nyota lakini mengi kukihusu bado hayajulikani.

"Utafiti zaidi utaruhusu wanaastronomia kubaini iwapo hili ni tukio la nadra kutokea au ni idadi kubwa ya watu ambayo haijawahi kuona hapo awali. Natumai kuelewa kitu hiki na kujua zaidi kuhusu hilo baadaye," alisema. Dk. Hurley-Walker.

CHANZO BBC SWAHILI

Post a Comment

0 Comments