SUAMEDIA

GENERAL DEFAO afariki Dunia

 

Defao afariki dunia baada ya kuripotiwa ugonjwa akiwa kwenye safari ya utumbuizaji Cameroon.


Taarifa zinasema Defao amefariki dunia siku ya jumatatu usiku katika Hospitali ya Laquintinie Hospital, Douala ambapo alipelekwa akiwa katika hali ya mahututi.

Siku tatu zilizopita mwanamuziki huyo alionekana akiwa amechoka katika chumba alichopumzikia baada ya kufanya onesho lake ndipo jeshi la polisi lilivunja mlango wa chumba hicho na baada ya hapo aliwahishwa hospitali kwa matibabu.

 Taarifa zisizo rasmi kutoka kwa vyanzo mbambali zimeeleza kuwa huenda mwanamuziki huyo atakuwa amepata maambukizi ya Corona.

Defao amefariki dunia akiwa Douala Cameroon, ambapo ratiba yake ilimtaka kutumbuiza kipindi cha usiku wa kuamkia mwaka mpya 2022.

Habari za General Defao zimetangazwa mapema 28th ya Dicemba 2021, kupitia Televisheni na Radio ya Taifa nchini Congo (RTNC).

RTNC ni kituo cha utangazaji cha Taifa jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo. ambayo iko chini ya Serikali.


CHANZO MUUNGWANA

Post a Comment

0 Comments