SUAMEDIA

Watanzania wameshauriwa kujifunza mafunzo ya udereva ili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika

Na Farida Mkongwe

Wananchi wa Mkoa wa Morogoro na watanzania kwa ujumla wameshauriwa kujifunza mafunzo ya udereva ambayo yamezinduliwa rasmi na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA ili waweze kupata weledi wa matumizi ya vyombo vya moto na barabara kwa lengo la kupunguza ajali zinazoweza kuepukika.

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Morogoro Bw. Abert Msando wakati wa ufunguzi wa shule ya udereva wa mitambo ya kilimo, magari na pikipiki uliofanyika Novemba 19, 2021 kwenye viwanja vya Kampasi ya Edward Moringe mjini Morogoro.

Bw. Msando amesema kuanzishwa kwa shule hiyo kutatoa nafasi kwa wananchi kupata mafunzo sahihi ya matumizi ya barabara pamoja na kuzijua alama za barabarani ukizingatia kuwa mafunzo hayo yanatolewa na wataalam.

“Mh. Mkuu wa Chuo mimi nina ombi la kuwa Mwanafunzi wa kwanza ambaye ninaenda kujifunza kwenye shule ya udereva wa mitambo ya kilimo hapa SUA, naomba nipewe control namba nikalipie, nijifunze mwanzo mwisho …… na nakuhakikishia nitafaulu”, alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Akizungmza na wanafunzi waliojitokeza kwenye ufunguzi huo Mkuu wa wilaya amesema ni vigumu wanafunzi kujifunza kupitia mitandao ya kijamii kama whatsapp au facebook na mingine na badala yake amewataka kujifunza kwa vitendo ili waweze kufanikiwa baada ya masomo yao.



  









Post a Comment

0 Comments