Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimesema katika kuhakikisha kinakabiliana na tatizo la jangwa katika nchi zilizoko Afrika na hasa ukanda wa Jangwa la Sahara watafiti wabobezi katika taalama ya misitu wataanza tafiti hivi karibuni katika nchi sita jambo litakalosaidia kukabiliana na matatizo mbalimbali yanayoikabili misitu hiyo
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala akisisitiza jambo kwa washiriki wa kongamano la kisayansi |
Akizungumza katika kongamano la kisayansi katika Programu hiyo ya ‘REFOREST’ lililowashirikisha wanafunzi wanaosoma Shahada ya Uzamivu katika fani ya misitu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala amesema nchi za Afrika zinahitajika kuwa na nguvu kazi mpya itakayosaidia kuondoa changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi
“Lengo kubwa ni kwamba tunaona nchi nyingi za Afrika zinakumbwa na tatizo la jangwa na hii ni kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na mambo mengine sasa hii inahitaji kuwa na nguvu kazi mpya ambayo itauondoa katika hili janga na ndiyo maana program hii inawafundisha wanafunzi 20 kutoka nchi sita za Afrika”
Prof. Mwatawala ameongeza kuwa wanafunzi watakapohitimu wanaweza kuipeleka elimu waliyoipata katika ngazi za chini kama Shahada ya Umahiri na Shahada ya awali
Naye Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii Prof. Suzan Augustino amesema wanafunzi hao watawasilisha maandiko ya tafiti ambazo wanaenda kufanya katika nchi zao ambayo yataangalia changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na usimamizi endelevu wa rasimali misitu
Amezitaja changamoto zingine ambazo wanafunzi hao watazifanyia kazi kuwa ni pamoja na kuangalia uwezo wa misitu kuhifadhi hewa ukaa ambayo imekuwa ni fursa na hasa kwa wananchi ambao wataiuza na kupata fedha wao na taifa pia na pia wataangalia mazao yatokanayo na misitu ikiwa ni pamoja na matunda mwitu na madawa
“Tunao wanafunzi ambao watakwenda kuangalia uwezo wa hii misitu yetu, kuweza kuhifadhi hii hewa ukaa ambayo imekuwa ni fursa hasa kwa wananchi watakaoiuza na kupata fedha lakini pia na taifa, biashara ambayo haijashamiri sana nchini lakini inakuja na lazima tujiandae, lakini lingine zuri zaidi wengine wanaenda kufanya tafiti katika miti ambayo tumeitumia lakini hatujaitumia sana ikiwemo mazao yale ya msituni na miti dawa”
Naye Mratibu wa Mradi huo wa ‘REFOREST’ kutoka SUA Prof. Roman Ishengoma amesema katika kuhakikisha SUA inatoa wahitimu bora watakaokuwa na ujuzi wa juu wa misitu wamehakikisha kila mwanafunzi anasimamiwa na waalimu watatu
“Pamoja na kuwafundisha darasani kuanzia Januari mwakani, wanatakiwa kila mmoja kurudi kwenye nchi yake kufanya utafiti na hatimaye kuandika andiko litakalompa shahada”
Prof. Ishengoma ameongeza kuwa katika kongamano hilo la siku 3 lililoanza Octoba 27, 2021 wamewaita walimu wanaowasimamia wanafunzi na kila mwanafunzi atawaeleza kuanzia mwezi Januari anaporudi nchini kwake atafanya utafiti wa namna gani, umelenga kutatua tatizo gani na atafanyaje
Wanafunzi zaidi ya 300 kutoka mataifa mbalimbali waliomba kusoma kozi hiyo ya Shahada ya Uzamivu ya Sayansi za Misitu ambapo wanafunzi 20 tu ndiyo waliofuzu huku watano ni Watanzania, watatu kutoka nchini Msumbiji, wanne kutoka nchi ya Rwanda, wanne kutoka Uganda, na wengine wanne ni kutoka Ethiopia kati ya hao 9 ni wanawake na 11 ni wanaume
Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii Prof. Suzan Augustino akizungumza na washiriki wa kongamano |
0 Comments