SUAMEDIA

Utendaji kazi na Tafiti zinazofanywa SUA kuchangia kupanda hadhi ya ubora Vyuo Vikuu Afrika

 

 

Na.Vedasto George.

Utendaji kazi uliotukuka pamoja na Tafiti mbalimbali zinazofanywa na Chuo cha Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA vimekiwezesha chuo hicho kuweza kupanda hadhi ya ubora kwa Vyuo Vikuu barani Afrika kutoka nafasi ya sitini na saba kwa mwaka jana hadi kufikia nafasi ya 53 kwa mwaka huu wa 2021.


Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof.Raphael Chibunda wakati akitoa salamu na kuzungumza na wanachama wa chama cha wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya juu,Sayansi,Teknolojia na Utafiti RAAWU Tawi la SUA katika  Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi duniani ambayo ufanyika kila ifikapo tarehe moja ya mwezi wa tano kila mwaka.

"Chuo chetu kimeweza kupanda hadhi katika vyuo vikuu vya afrika tulikuwa chuo cha sitini na saba mwaka jana lakini januari ya mwaka huu wa 2021 tumekuwa wa 53 ambapo kwetu tumeona ni mabadiliko makubwa lakini lengo letu ndani ya miaka miwili inayo kuja ni kuweza kuingia kwenye listi ya vyo vikuu ishirini bora."Alisema Prof.Raphael Chibunda

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu,Sayansi,Teknolojia na Utafiti RAAWU Tawi la SUA Bi.Gaudensia Donati amebainisha kuwa maadhimisho hayo ya siku ya wafanyakazi Duniani uadhimishwa   ili kukukbuka harakati za kudai haki kwa wafanyakazi zilizopelekea kuundwa kwa Vyama vya wafanyakazi ambavyo msingi wake mkubwa ni kuweka mazingira mazuri maala pakazi na kuweza kujadiliana na mwajiri ili wafanyakazi waweze kilipwa ujila wao sahihi.

"Hapo zamani wafanyakazi walikuwa wanafanya kazi nzito wanatumikishwa lakini walikuwa wanapewa ujira mdogo usio kidhi mahitaji yao na kwa nchi yetu kamanda ambaye tunamkumbuka aliweza kupambana na kudai haki za wafanyakazi na vuguvugu la vyama vya wafanya kazi ni hayati Mfaume Kawawa yeye ndiye alifanya vuguvugu kubwa na alihangaika sana kuona Tanzania kunakuwa na msingi wa vyama vya wafanyakazi ili nao waweze kuongea na mwajiri" Alisema Bi.Gaudensia Donati.

Naye Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu,Sayansi,Teknolojia na Utafiti RAAWU Tawi la SUA Bi.Catherine Ogessa amekiomba Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kuendelea kudumisha utawala bora katika kutatua kero za wafanyakazi  ikiwemo kuboresha mazingira ya kazi kwa maana ya vitendea kazi na usalama kazini.

Katika kutambua mchango na kazi kubwa inayofanywa na wafanyakazi katika Chuo hicho cha SUA kimetoa tunzo kwa wafanyakazi bora 56 kati yao sita ni wafanyakazi hodari.

Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi kwa Mkoa wa Morogoro yamefanyika Manispaa ya Morogoro yakibebwa na kauli mbiu isemayo MASILAHI BORA, MISHAHARA JUU KAZI IENDELEE, wito ukitolewa kwa serikali kuangalia namna bora kuboresha mishahara na madaraja ya wafanyakazi na kudhibiti ukandamizaji kwa wafanyakazi kwa baadhi ya taasisi.


 


Post a Comment

0 Comments