SUAMEDIA

Chad yajiandaa kwa mazishi ya Rais Deby huku huku viongozi wakiwasili

 Mazishi ya kitaifa ya Rais wa Chad Idriss Déby Itno yatafanyika Ijumaa katika mji Mkuu wa nchi hiyo N'Djamena kabla ya kuzikwa katika mkoa wake.




Aliuawa Jumatatu katika eneo la mapigano dhidi ya wapiganaji wa Front for Change and Concord in Chad (Fact), kikindi cha wanajshi kilichoundwa na maafisa wa kijeshi mwaka 2016.

Viongozi wa mataifa ya Mali na Guinea wamewasili, na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pia anawasili kuelekea mjini N'Djamena licha ya onyo kutoka kwa waasi kwamba kiongozi huyo wa kigeni hapaswi kuhudhuria kwa sababu za kiusalama.

Baada ya kutolewa kwa heshima za kijeshi na hotuba mbali mbali, sala itafanyika katika msikiti wa Grand Mosque uliopo N'Djamena.

Baadaye , mwili wa Bw Déby's utasafirishwa kwa ndege hadi Amdjarass, kijiji kidogo kilichopo karibu na mji anakotoka wa Berdoba, uliopo zaidi ya kilomita 1000 (maili 621) kutoka mji mkuu, karibu na mpaka wa Sudan.

Rais Déby alikuwa mtu muhimu katika mkakati wa usalama katika kanda ya Sahel.

Baraza la kijeshi linaloongozwa na mwanae, Jeneral Mahamat Idriss lilichukua madara baada ya kifo chake naanaungwa mkono kwa kiasi kidogo na jeshi lakini anauungwa mkono na mtawala wa Ufaransa.

Generali Déby, 37, amesema jeshi litafanya uchaguzi wa kidemokrasia katika kipindi cha miezi 18 ijayo, lakini viongozi wa upinzani wamelaani hatua yake ya kuchukua mamlaka na kuitaja kama mapinduzi na jenerali wa kijeshi amesema maafisa wengi wanapinga uongozi wake wa mpito.

Ni mpango ambao pia waasi waliupinga huku pia wakionya kuwa watasitisha kipindi kidogo kilichokuwepo cha usitishaji mpigano.

Mgawanyiko ndani ya jeshi na upinzani vinamaanisha kuwepo kwa ukosefu mkubwa wa usalama huku kukiwa piwa nma changamoto za kiuchumi wakati Chad inaingia katika kipindi cha mpito .

CHANZO BBC SWAHILI

Post a Comment

0 Comments