Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya moyo.
Rais Magufuli alifikishwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Machi 6 mwaka huu na kuruhusiwa Machi 7, akaendelea na majukumu yake.
Hata hivyo, alipelekwa katika Hospitali ya Mzena Machi 14 baada ya kueleza kujisikia vibaya, ambapo amekuwa akipatiwa matbabu hadi umauti ulipomkuta.
Kufuatia msiba huo, Makamu wa Rais ametangaza siku 14 za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti.
0 Comments