SUAMEDIA

Morogoro yakumbwa na changamoto ya Miundombinu ya Elimu

 

Na.Vedasto George.

Mkoa wa Morogoro unakabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa, vyoo, nyumba za walimu pamoja na madawati na kupelekewa kuwepo kwa msongamano mkubwa wa wanafunzi katika shule za msingi na Sekondari.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Olesanare katika Kikao cha Kamati ya Ushari ya Mkoa  wa Morogoro (RCC) 


Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa huo Loata Olesanare katika kikao cha kamati ya ushari ya mkoa RCC na kusema kuwa katika shule za sekondari kuna upungufu wa vyumba vya madarasa miatatu tisini na tisa 399 nyumba zawalimu elfu nne miamoja sitini na moja 4,161matundu ya vyoo upungufu ukiwa ni Elfu mbili miamoja harobaini na saba 2,147.

“Bila kuondoa upungufu wa miundombinu katika shule zetu watoto wetu watakosa haki yao yamsingi ya elimu bora nielekeze wakuu wa Wilaya na wakurugenzikatika halmashauri zote kusimamia miundombinu ya shule za msingi na sekondari” Alisema Loata Ole Sanare.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameleeza kuwa katika kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2016 hadi kufikia mwaka 2019 wanafunzi wapatao elfu moja miamoja na tisini nanne 1,194 katika Mkoa wa Morogoro  wamepata mimba  za utotoni na kukatiza masomo yao.

“Mkoa kwa miaka mine idadi ya wanafunzo waliopata mimba ni1,194  tatizo ni kubwa na kwamaana hiyo nitoe wito kwa wenzetu wote na vyombo mbalimbali wachukue hatua  za kisheria juu ya tatizo hili hali hii haikubaliki kwa namna yeyote ile  nadani ya mkoa wa Morogoro, niwaelekeze Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi kushirikiana na vyombo vingine vya usalama kuakikisha wote wanaowapa watoto shule mimba  kuakikisha wanachukuliwa hatua.” Alisema Loata Ole Sanare.

Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro Eng. Joyce Baravuga amesema Mkoa tayari umeweka mikakati maalumu itakayowezesha kuimalisha ufaulu ikiwemo kutumia mifumo ya TEHAMA katika ufundishaji, kuimalisha mifumo mbalimbali ya ufundishaji na kujifunzia kwa wanafunzi pamoja  na kuhamasisha wadau wa elimu kuendelea kujitokeza  kuchangia katika sekta hiyo ya elimu.

Katika  hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ametoa mwezi mmoja kwa wakuu wa wilaya, wakurugenzi kukamilisha ujenzi wa vituo vya afya na Zahanati  katika maeneo yao na kusema kuwa kiasi cha shilingi bilioni 14 .7 zimetumika kufanya ukarabati  wa hospitali za zamani mbili na  Zahanati moja  katika kipindi cha kuazia mwaka 2016 mpaka mwaka 2021.

Kikao cha Kamati ya Ushari ya Mkoa wa Morogoro kimewajumuhisha wakuu wa wilaya zote za mkoa huo, wakurugenzi kamati ya ulinzi na usalama mkoa, watumishi pamoja na wadau wengine wa maendeleo mkoani humo lengo likiwani kujadili na kutathimini kazi za maendeleo  zilizofanyika mkoani morogoro.

 

 

 

Post a Comment

0 Comments