Na.Vedasto George,
Vyuo Vikuu Nchini
vimetakiwa kuzalisha wanafunzi wabunifu na wazalendo ambao wataweza kwenda kubuni miradi mbalimbali
ambayo itawawezesha kujiajiri na kuajiri wengine ili kuweza kutatua changamoto ya upatikanaji wa ajira nchini
pindi wanapohitimu masomo yao ya elimu ya juu.
Prof. Mkumbo amesema kwa
sasa nchi inahitaji vijana wabunifu na wazalendo ambao watakuwa chachu katika kuwekeza katika miradi mbalimbali ikiwemo ya
kilimo ,ufugaji, na uvuvi huku akiweka msisitizo kwa vyuo vikuu nchini kuwa na
utaratibu wa kuwaandaa vijana katika kuwafundisha zaidi namna ya kujiajiri
pasipo kusubiri ajira kutoka serikalini.
Aidha Prof. Mkubo ameongeza
kuwa wanafunzi kumi wanaohitimu elimu ya juu ni watano tu ambao wanaweza
kuajiriwa huku wanafunzi wengine zaidi
ya asilimia 10 wakiwa wanabaki mtaani wakiwa hawana kazi wala ujuzi wa
kujiajiri.
“Lazima tubadilike kwenye ufundishaji wetu na tujue wanafunzi wanasoma nini ,kwa sasa dunia imebadilika tunaitaji vijana wanaoweza kujiajiri kwa hiyo sisi kama taasisi inayotoa elimu lazima tuwaandae vijana wetu zaidi kwenye kwenda kujiajiri, tukiweza kufanya hivyo na vijana wetu wakaelewa basi taifa letu litaondokana na changamoto ya ukosefu wa ajira” alisema Prof. Kitila Mkumbo
Kwa upande wake Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo upande wa Taaluma Prof. Maulid
Mwatawala amesema SUA ni miongoni mwa vyuo ambavyo vinawaandaa wanafunzi zaidi
kwenye kujiajiri na kusema kuwa SUA
itakuwa mfano wa kuigwa nchini.
“Mh. Waziri nikuakikishie tuko vizuri, wanafunzi wote wanaosoma masuala ya kilimo, mifugo, uvuvi na masuala ya utalii hawa wote tunawaandaa ili waweze kujiajiri”alisema Prof. Maulid Mwatawala
Katika mkutano Waziri wa
Nchi,Ofisi ya Rais (Uwekezaji) Prof. Kitila Mkumbo amemkabidhi mwanafunzi Musa Gese Doto tuzo
mbili tuzo ya Mbunifu Bora wa Teknolojia ambapo amebuni gari shamba tuzo ambayo
imetolewa na SETO TV na tuzo ya mbunifu bora wa Mwaka 2020 ambayo imetolewa na
Tanzania Universities and Colleges Students Awards
KATIKA PICHA
0 Comments