SUAMEDIA

Mheshimiwa Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba awatunuku Wahitimu 2943 SUA

Na: Catherine Mangula Ogessa.

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kimefanya Mahafali yake 36 ambapo Mkuu wa Chuo hicho  Mheshimiwa  Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba amewatunuku jumala ya wahitimu 2943 katika Program mbalimbali.



Kama ilivyo kawaida ya Mahafali, Mkuu wa Chuo hicho awali amekaribishwa  na Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof, Raphael Chibunda kuunda rasmi mkusanyiko huo kuwa Mahafali ya Chuo Kikuu kwa Minajili ya kutunukisha Shahada, Stashahada na Astashahada za Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo.

Katika Mahafali ya mwaka huu idadi ya wahitimu wa kike imeongezeka na kufika wahitimu 1097 tofauti na ile ya mwaka 2019 ambapo wahitimu wa kike walikuwa ni 874.

Katika hotuba yake Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman kwanza kabisa ameishukurua Serikali kwa jinsi ambavyo imekuwa ikitoa Ruzuku kwa Chuo hicho na hivyo kuwezesha kutekeleza majukumu makuu ya chuo hicho ambayo ni utoaji wa mafunzo, kufanya Utafiti, kutoa huduma pamoja na kuzalisha mali.

Mbali na hayo mwenyekiti huyo wa Baraza pia amewapongeza wahitimu kwa kuhitimu , lakini pia walimu, pamoja na wazazi au walezi waliofanikisha katika safari yao ya masomo lakini ametumia muda huo  kuwaasa wahitimu wote.

 Kwa upande wake Makamu mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda  amebainisha kuwa ni ukweli usio fichika kuwa shule ya Sua haijawahi kuwa lele mama hivyo ni imani kwake mafanikio ya elimu waliyoipata itakuwa ni tija kwao na kuleta ufanisi kwa taifa huku akiwasisitiza kuacha ulalamikaji na badala yake wakawe wabunifu, wajasiriamali ili wakalete tija kwao wenyewe, jamii na taifa kwa ujumala.

Katika hatua nyingine Prof. Chibunda ameelezea namna wanavyokabiliwa na changamoto lakini pia wanafanya kila iwezekanavyo kuzitatua.






Post a Comment

0 Comments