Na Gerald Lwomile
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA na
Waziri Mkuu Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba amewataka watafiti kutoka
SUA kumsaidia mkulima mdogo kuzalisha kwa tija huku akitumia mbinu bora za
kilimo ili nchi iondokane na umaskini.
Jaji Warioba amesema hayo wakati akihitimisha ziara
yake ya siku mbili leo Novemba 18, 2020 katika kampasi ya Mazimbu na Kampasi ya
Edward Moringe zamani ikijulikana kama Kampasi Kuu.
Warioba amesema jitihada zinazofanywa na SUA ikiwa ni pamoja
na uanzishaji wa mashamba darasa na kituo Atamizi ambacho kinafundisha mbinu za
kilimo biashara kwa kutoa mafunzo, ushauri na mbinu bora za kilimo kwa kiasi
kikubwa kama kutakuwa na muitikio kwa vijana na wananchi kwa ujumla inawezekana
kabisa kuondoa umaskini kwa wananchi wengi.
Amesema shamba darasa la SUA limeonyesha mafanikio
makubwa kwani mbali na kuzalisha lakini imekuwa sehemu ambayo wanafunzi
wanajifunza kwa vitendo kulima na kuhudumia mazao mbalimbali ya kilimo, ufugaji
na uvuvi.
“nisema kuwa mafunzo yale yanayofanywa katika shamba
darasa na kituo Atamizi ile ni mbegu nzuri sana sio kusaidia vijana tu lakini
kubadili kilimo chetu, kwa sababu watakwenda pale na kujifunza kilimo lakini
pia biashara na kama kweli tunataka kuondoa umaskini ni lazima tufanye hali ya
mkulima mdogo iwe na tija zaidi” amesema Jaji Warioba.
Akizungumzia maendeleo ya chuo Mkuu wa chuo hicho Jaji Warioba amesema pamoja
na kuwepo kwa matatizo ya rasimali mbalimbali lakini chuo kimejitahidi
kuhakikisha chuo kinakuwa katika hali ya usafi na kuhakikisha ukarabati
unafanyika katika majengo na barabara.
Mkuu wa Chuo Jaji Mstaafu Warioba na Mwenyekiti wa Baraza wakisikiliza maelezo juu ya ufugaji wa samaki
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoine
SUA Jaji Mkuu Mstaafu Chande Othman amesema zaidi ya shilingi Bilioni 21
zimetumika katika mpango mkakati wa chuo wa awamu ya nne ambao ulianza mwaka
2016 na unataraji kukamilika mwaka 2021 ambapo utekelezaji wake umekuwa kwa asilimia
zaidi ya 74.
“kuna mazuri mengi ambayo tumefanya lakini kuna ambayo
tunatakiwa kuhitahidi moja ni suala la jinsia, lakini pia kuna hatua chuo
kimepiga katika ugani lakini pia kuna suala uratibu” amesema Jaji Mkuu Mstaafu
Chande.
Mkuu wa Chuo Jaji Mstaafu Warioba na Mwenyekiti wa Baraza wakisikiliza maelezo kutoka kwa Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Chibunda juu makaburi ya kihistoria ya wapigani uhuru wa Afrika ya Kusini
Akizungumzia namna chuo kinavyoendelea kutanua huduma
zake katika maeneo mbalimbali nchini Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo SUA amesema tayari wameanzisha kampasi katika mkoa wa Katavi inayojulikana
kama kampasi ya Mizengo Pinda
Amesema kuanzia mwaka huu wa masomo kampasi hiyo
itatoa programu tatu ambazo ni shahada ya utunzaji wa rasilimali nyuki, Astashada
ya kilimo na lakini pia watatoa mafunzo katika ngazi ya cheti katika fani ya
kuongoza watalii na uwindaji
“ili tuweze kufundisha vizuri tumeshafanya uamuzi kuwa
sasa kufundisha kwa nadharia tu hivyo tutafundisha zaidi kwa vitendo kwa hiyo
tumeshapeleka trekta, trela pamoja na opareta kwa ajili ya kufungua shamba la
mafunzo katika kampasi hiyo lakini pia tumemaliza ujenzi wa shamba darasa la
nyuki na tayari tuna mizinga sabini ambayo ina nyuki kwa hiyo wanafunzi
wanapoanza mwaka huu watatumuia mashamba hayo kujifunzia” amesema Prof.
Chibunda
Ziara ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilmo SUA
imefanyika kwa siku mbili ambapo amejionea miradi mbalimbali ya maendeleo kama
ujenzi wa miundombinu, maabara mbalimbali ikiwemo maabara mtambuka, shamba darasa,
maabaya ya sayansi kampasi ya Mazimbu, Kituo Atamizi na Hospitali ya Rufaa ya
Wanyama
Mkuu wa Chuo Jaji Mstaafu Warioba na Mwenyekiti wa Baraza wakisikiliza maelezo kutoka Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Chibunda juu kijana mbunifu aliyekaa kwenye gari ambaye ndiyi aliyebuni shamba gari hilo
0 Comments