SUAMEDIA

Miche matunda na migomba inayozalishwa kwa njia ya chupa SUA kivutio katika Maonesho ya TCU

 

Na: Tatyana Celestine

Miche ya Matunda na migomba inayozalishwa kwa njia ya chupa katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA umekuwa kivutio kikubwa  katika banda la chuo hicho kwenye Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea jijini Dar es salaam


Mbali na kufanya udahili wa wanafunzi, pamoja na kutoa ushauri kwa wanao taka kujiunga na SUA , chuo hicho kimeendelea kutoa  elimu yenye fursa nyingi katika kujiajiri na  kuajiriwa  kutokana na teknolojia sahihi inayotumika katika uzalishaji wa mazao mbalimbali kupitia Idara ya Sayansi ya Mimea na Mazao ya Vipando chuoni hapo.


Akizungumza na SUAMEDIA katika Maonesho  hayo ya Vyuo Vikuu  Mwalimu Caroline Marwa kutoka Idara ya Sayansi ya Mimea na Mazao ya Vipando  amesema  kazi kubwa ya kutoa elimu kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na chuo imezaa matunda kwa kuwa wanafunzi wengi wametambua kile ambacho kinatolewa SUA na kwamba atakapomaliza chuo atakwenda kufanya kazi gani kulingana na kozi anayoichagua.

"wanafunzi wengi wanakuja wakiwa hawajui kozi zipi zinatolewa na SUA kazi tunayoifanya ni kuwaelekeza kila kitu kwa ufasaha zaidi ili waweze kutambua na kujiunga na chuo", alisema Mwalimu Marwa

 

Bi. Marwa ametoa wito kwa  wazazi na wananchi kwa ujumla watambue kuwa SUA inafundisha matumizi ya Teknolojia ambazo zinaweza kuzalisha mazao bora kwa wingi na yanayopambana na magonjwa hivyo mwanafunzi akijiunga na chuo hicho atatumia Teknolojia hizo hata pasi kuajiriwa

Tumekuja na miche michache kwasababu SUA tunazalisha miche lakini tumeshangaa kuona kuwa sasa ni mvuto wao na hatuwezi kuwaletea hapa hivyo watu waweke oda watatumiwa, alisema Mwalimu Marwa





 

Post a Comment

0 Comments