Na: Tatyana Celestine
Kituo cha TEHAMA katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA
kimewahahakishia wanafunzi watakaojiunga na chuo hicho kuwa usajili wao kwa
njia ya tehema ni wa uhakika maana wamejiandaa vyema kufanya kazi hiyo.
Akizungumzia idadi ya wanafunzi wanaokuja kwa siku na jinsi ya wanavyokabiliana nao kwa udahili Dkt. Churi amesema kuwa chuo kimepeleka idadi ya kutosha ya wafanyakazi ili kurahisisha zoezi hilo linaloendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Ameongeza kuwa Kituo cha TEHAMA kimejiimarisha katika miundo mbinu ya kufundishia na kuwata wanafunzi wanaokidhi vigezo kujitokeza kwa wingi wakiwemo wale wanaotaka kujisomea kupitia njia mtandao
“Nawakaribisha kwasababu chuo chetu kimejihimarisha vizuri ikiwa ni pamoja na mtandao unaotosheleza kielimu, kupata kusoma vitabu na maabara zipo za kutoasha kwa ajili ya waafunzi ivyo tuna wakariisha sana sua” alisema Churi.
0 Comments