SUAMEDIA

USINDIKAJI NI NJIA BORA YA KUOKOA MATUNDA YANAYOHARIBIKA KWA HARAKA


Na:Farida Mkongwe
Wakulima nchini wameshauriwa kusindika mazao yao yakiwemo
mazao ya matunda ambayo hayana uwezo wa kukaa muda mrefu
bila kuharibika ili kuyaongezea thamani mazao hayo.

Ushauri huo umetolewa na Afisa Mkuu wa Maabara, Idara ya
Teknolojia za chakula, Sayansi za Lishe na Walaji kutoka Chuo kikuu
cha Sokoine cha kilimo SUA Bi. Gaudencia Mchotika wakati
akizungumza kwenye kipindi cha karibu Mezani kinachorushwa
hewani na SUAFM.

Bi. Mchotika amesema mazao mengi ya matunda yakiwemo mapapai
hayawezi kukaa muda mrefu bila kuharibika lakini yakisindikwa yana
uwezo wa kumpatia kipato mkulima na pia yanaweza kuuzwa kwa bei
kubwa kwa kuwa yameongezewa thamani.

Akitolea mfano wa mapapai, amesema matunda hayo hayapendwi
sana kama ilivyo kwa matunda mengine lakini kwa njia ya kuyasindika
na kutengeneza bidhaa nyingine kama jam au chachandu watu wengi
wamekuwa wakiyapenda na hivyo kununuliwa kwa wingi.

Afisa Mkuu huyo wa Maabara, Idara ya Teknolojia za chakula, Sayansi
za Lishe na walaji kutoka SUA amewataka wakulima kujifunza
teknolojia hiyo ya usindikaji na kuitumia mara kwa mara ili
kuepukana na hasara inayosababishwa na mazao ya matunda
kuwahi kuharibika.

Post a Comment

0 Comments