SUAMEDIA

Ushuru wa nywele za bandia wapandishwa

Serikali kupitia Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango imependekeza kupandisha kwa ushuru wa asilimia 10 kwa bidhaa za nywele bandia zinazozalishwa nchini na asilimia 25 kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje nchi.



 Akizungumza Bungeni jijini Dodoma Waziri Mpango ameeleza kuwa "napendekeza kutoza ushuru wa asilimia 10 kwenye bidhaa za nywele za bandia, zinazotengenezwa ndani ya nchi na asilimia 25 zazoagizwa kutoka nje ya nchi lengo ni kuongeza mapato ya Serikali."


Pendekezo hilo limetolewa na Dkt.  Mpango wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020.


Mara baada ya Waziri Mpango kuwasilisha pendekezo hilo kwenye bajeti ya Serikali, ukumbi wa Bunge uliripuka kwa kelele kwa Wabunge wakipiga meza zao wakionesha kufurahia pendekezo hilo.


Chanzo: MILARD AYO

Post a Comment

0 Comments