SUAMEDIA

SUA yaelezea mafanikio ya Mradi wa HEET

 

Na: Farida Mkongwe

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi  na Teknolojia kwa kuleta Mradi wa Elimu ya Juu  kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) ambao umeleta tija Chuoni hapo.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Utawala na Fedha SUA Prof. Amandus Muhairwa akifungua Mkutano wa Wadau katika utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu  kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).


Kauli hiyo imetolewa Agosti 21, 2023 na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Utawala na Fedha SUA Prof. Amandus Muhairwa wakati akifungua Mkutano wa Ushirikishwaji wa Wadau wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi uliofanyika Chuoni hapo.

Prof. Muhairwa amesema kupitia mradi huo unaohusisha ushirikiano wa Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania, Chuo kimepata jumla ya Tsh. Bilioni 73.8 ambazo zitatumika ndani ya miaka 5 kuanzia 2021-2026 ambapo zaidi ya nusu ya fedha hizo zinatumika kwa ajili ya kuboresha upande wa taaluma na shughuli za utawala.

“Fedha hizi pia zitatumika kuongeza jengo kwa ajili ya madarasa katika Kampasi yetu ya Katavi na mabweni ikiwa ni mpango wa Sera ya Serikali kuhakikisha kila mkoa nchini unakuwa na Chuo Kikuu au Tawi la chuo kikuu litakalowawezesha wanachuo kupata elimu iliyo bora”, amesema Prof. Muhairwa. 

Amesema pamoja na fedha hizo kutumika kuongeza maabara ambazo zitaboresha mazingira ya kusoma na kufundishia, mpaka sasa wamefanikiwa kuwapeleka masomoni ndani na nje ya nchi walimu 41 wanaosoma Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu.

Prof. Muhairwa ameeleza mafanikio makubwa ya mradi huo yatategemea ushiriki wa wanajumuiya wote wa SUA ambapo ametoa wito kwa wadau walioshiriki mkutano huo kuyaelewa 

Baadhi ya Wadau walioshiriki katika Mkutano wa Wadau katika utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu  kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) SUA.







Post a Comment

0 Comments