Na: Calvin Gwabara – Dar es salaam.
Menejimenti ya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) imefanya ziara ya mafunzo kwenye Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ili kuongeza mahusiano na kujifunza mifumo mbalimbali inayotumiwa na ofisi hiyo.
Akizungumza katika ziara hiyo, Kaimu Mwandishi Mkuu wa Sheria Bi. Rehema Katuga amesema lengo la ziara hiyo ni kuitambulisha ofisi hiyo mpya na viongozi wake, kujifunza namna wanavyotumia mifumo mbalimbali ya kielektronic inavyofanya kazi pamoja na kudumisha ushirikiano baina ya Ofisi hizo mbili zinazotegemeana katika majukumu yao.
“Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, kama unavyofahamu ofisi yetu ni mpya imeanza
rasmi mwezi wa saba mwaka huu, hivyo kuna mifumo mingi ya kiutendaji ya
kielektroniki inayotumika katika utekelezaji wa majukumu na utawala ambayo na
sisi tunapaswa kuwa nayo lakini tumeona ni vizuri kuja kujifunza kwenu namna
inavyofanya kazi, faida zake na changamoto zake ili tunapoanza kuitumia basi
tuwe na uelewa mpana ndio maana tumekuja na wataalamu wetu wote” Alisema Bi.
Katuga.
Aidha
ameongeza kuwa malengo ya OCPD ni kuhakikisha inaachana na matumizi makubwa ya
kutumia karatasi kwenye shughuli mbalimbali za kiutendaji kwenye idara na
vitengo kwa kutumia mifumo hiyo ya kielektroniki.
“Tumedhamiria
kuhakikisha shughuli zote za taasisi kuanzia idara ya fedha, utawala na
manunuzi na Idara za uandishi wa sheria zinatumia mifumo katika kutekeleza
majukumu yake, aidha tungependa kuona mifumo hiyo inasomana ili
kurahisisha utendaji wa Ofisi yetu” alifafanua Bi. Katuga.
Bi. Katuga ameishukuru Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa ushirikiano mkubwa
wanaoupata katika utekelezaji wa majukumu yake na kuwasihi wasisite
kuwatatafuta pale wanapokuwa na changamoto yoyote katika tafsiri ya sheria
yoyote kwakuwa wao OCPD ndio wanaoziandika wanaweza kutoa ufafanuzi sahihi.
“
Kiukweli OCPD na OSG ni ofisi ambazo zinategemeana sana maana sisi OCPD
tunaandika sheria zote za nchi lakini watumiaji ni nyinyi Ofisi ya Wakili Mkuu
wa Serikali hivyo tupo tayari wakati wowote kuwasaidia pale mnapokumbana na
Changamoto ya ufafanuzi wa sheria hizo msisite kutuona maana tunazijua vizuri
zote” Alisema Bi. Katuga.
Kwa upande wake Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Alice Mtulo amewapongeza kwa kuchagua ofisini yao kuwa mahali pazuri pa kujifunzia mifumo ya kiutendaji ya kielektroniki inavyofanya kazi na kuwaahidi ushirikiano ili waweze kupata taarifa zote wanazohitaji.
Amesema Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) na Ofisi ya Wakili Mkuu wa
Serikali (OSG) ni kama ndugu maana wanategemeana kwenye mambo mbalimbali ya
utekelezaji wa majukumu hivyo anaamini wataweza kuendeleza ushirikiano huo
katika nyanja mbalimbali za utoaji wa huduma.
“Niwahakikishie kuwa tumejipanga vizuri kwa kuwakutanisha mbele yenu na
wataalamu wetu wote ambao wanashughulika na mifumo hiyo hivyo mtapata muda
mzuri wa kuuliza maswali yote mnayotaka na kupata majibu yatakayosaidia
kutimiza lengo la ziara yenu na tunayo mifumo mingi ambayo intumiwa na Serikali
na mingine ya ndani ambayo mtaiona yote” Alisema Bi. Alice.
Ziara hiyo ya kimafunzo inajumuisha wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali vya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria ambayo ina lengo la kujifunza kwa kina namna baadhi ya Ofisi za Serikali zinavyotumia mifumo hiyo kabla ya kuanza kutengeneza mifumo yake.
MATUKO KATIKA PICHA WAKATI WA MAJADILIANO.
![]() |
| Kaimu Mwandishi Mkuu wa Sheria Bi. Rehema Katuga akieleza lengo la ziara hiyo. |
![]() |
| Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Alice Mtulo akitoa neno la ukaribisho kwa menejimenti ya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa sheria (OCPD). |
![]() |
| Kaimu Mkurugenzi wa Divisheni ya Utawala na Rasilimali Watu (OCPD) Bi. Betlanda Msolla akichangia jambo wakati wa mjadala huo hasa kuhusu mifumo ya kiutawala inavyofanyakazi kwenye ofisi hiyo. |
![]() |
| Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Disheni ya Uandishi wa sheria (OCPD) Bi.Chresensia Mathayo akizungumza jambo wakati wa majadiliano na wataalamu wa ofisi ya Wakili Mkuu wa Sheri. |
![]() |
| Bw. Francis Adolf ambaye ni Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani kutoka OCPD akichangia kwenye majadiliano hayo. |
![]() |
| Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Alice Mtulo (wa kwanza kushoto) akizungumza wkati wa majadiliano. |
![]() |
| Bw. Alfred Nyaronga amabye ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (OCPD) akifafanua kuhusu mifumo wanayolenga kijifunza kutoka OSG. |
![]() |
| Menejimenti ya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria wakifuatilia mawasilisho kuhusu mifumo ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali inavyofanyakazi. |










0 Comments