Na: Ngolo Mboje
Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali
ikiwemo Ofisi ya Uhamiaji mkoani Morogoro, kimetoa elimu na kuwapongeza
wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliojiunga na chuo hicho kwa mwaka wa masomo
2025/2026.
Akizungumza
katika mkutano uliofanyika katika Kampasi ya Edward Moringe Sokoine, November
17 2025 Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano
na Masoko wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo ( SUA) Bi. Suzan Magobeko, amewaapongeza
wanafunzi hao na kuwataka kuwa mabalozi wazuri wa chuo, hususan kupitia
mitandao ya kijamii.
Aidha,
Kaimu Mkuu Mlezi wa Idara ya Ushauri kwa Wanafunzi SUA, Bi. Hilda Gamuya, amesema
kuwa mwitikio wa wanafunzi wa mwaka huu ni mzuri tofauti na mwaka wa masomo
2024/2025, kwani wana imani kuwa elimu wanayoitoa inaweza kuleta hamasa na
mtazamo chanya ili kuendana na utaratibu wa chuo.
Bi. Hilda
ameongeza kuwa matarajio yao makubwa ni kuona wanafunzi wanabadilika na
kuendana na utaratibu, sheria na kanuni za chuo, lengo likiwa ni kuwajengea
misingi bora ya maisha wawapo katika kampasi chuoni hapo.
Kwa
upande wake, Afisa Usajili wa Mkoa wa Morogoro, Bw. James Malimo, ameeleza
umuhimu wa wanafunzi kuwa na namba ya NIDA, akisema kuwa namba hiyo itawasaidia
kupata huduma mbalimbali ikiwemo huduma za afya, mikopo, pamoja na kuepusha
usumbufu wa kukosa huduma muhimu kwa wakati.pia itawasaidia kutambulika
Aidha,
Bw. James ametoa wito Kwa wanafunzi hao kutoa taarifa sahihi wakati wa mchakato
wa usajili, kwani taarifa hizo zitawasaidia katika masuala ya elimu na maisha
yao kwa ujumla.na kuwataka wajitokeze kwa wingi kujisajili.
Nao
wanafunzi wa mwaka wa kwanza, Bi. Laisa Bakari na Robert Laurent, walieleza
namna walivyopokelewa chuoni hapo, wakisema mapokezi yao yamekuwa mazuri na
kwamba elimu waliyopewa itawasaidia kufuata sheria, kanuni na utaratibu wa
chuo. Aidha, wamesema matarajio yao ni kuanza masomo yao rasmi kwa mafanikio.




0 Comments